Tanzania na mfumo wa unadhimu wa vyama bungeni

Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
2,213
1,638
Mwaka 1992 tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi Serikali iliona kuna haja ya kubadili mfumo wa kufanya maamuzi bungeni ili uendane na huo mfumo wa vyama vingi. Mfumo huo ukabadilishwa nasi tukaingia katika mfumo wa unadhimu wa vyama.

Lengo la mfumo huu ni kuhakikisha kwamba vyama vinapata nafasi ya kufanya maamuzi kupitia wabunge wake.

Ni mfumo ambao vyama huwataka wabunge wake wengi, kama sio wote, waweko bungeni wakati bunge likiamua swala lenye umuhimu. Aidha katika mfumo huu vyama hutoa maelekezo kwa wabunge juu ya namna ya kuamua swala fulani muhimu. Katika lugha nyepesi ni kwamba mfumo unaweka ile dhana ya chama kushika hatamu bungeni.

Wabunge huelekezwa swala lililoko mbele yao ama waliamue kwa kuangalia chama kina msimamo gani juu ya swala hilo, au huamua mbunge afanye maamuzi kwa kiuangalia matakwa ya wapiga kura wake, au waamue kwa namna mbunge mmoja mmoja wanavyoona wao kama wabunge. Wabunge wanaoenda kinyume na maagizo hayo wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ndani ya chama husika.

Upande mwengine, lengo la kuweko mbunge katika jimbo ni kuwatetea wapiga kura wake. Hili linamfanya mbunge afanye maamuzi kulingana na maelekezo ya wapiga kura wake kwani wao huwa wanamchagua mbunge aende bungeni akawawakilishe, awasemee mambo yao na hivyo kutekeleza maagizo yao.

Hali hii ya wapiga kura kusemewa na mbunge huwa inafinywa katika mfumo huu na badala yake chama kinashika hatamu na kuwa ndio wafanya maamuzi kwa mlango wa nyuma (indirectly).

Kwa maoni yako unadhani mfumo huu uendelee au ubadilishwe? Kama ungependa ubadilishwe hebu toa maoni ya nini cha kufanya.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom