MwajabuOmary
JF-Expert Member
- Jul 11, 2013
- 2,038
- 2,948
Kupitia mijadala mbalimbali na hasa baada ya TAML kukamatwa na kufunguliwa shitaka la uhaini kumekua na mijadala mingi sana na nilichogundua ni kwamba watu wengi hawajielekezi kwenye kanuni za uhaini.
Ili uhaini utendeke vipo vipengele kadhaa (principles) vikamilike ndio waweza kumtia mtuhumiwa hatiani. Kwa mfano kosa la WIZI.
Katika kosa hili ,ili lionekane ni kosa, vipo vitu vitatu mahakama lazima ijiridhishe kama ifuatavyo:
1. Kitu kinachodhaniwa kuibiwa lazima kiwe na thamani,
2. Kiwe kinahamishika
3. Kiwe na mmiliki
Lkn mwisho tena kwa umuhimu lazima uwepo wa nia ovu ithibitike.
TUJE KWE KOSA LA UHAINI,
tafadhali hapa naitoa kama ilivyo kwa mujubu wa kifungu kilivyo na sio maneno yangu.
KOSA LA UHAINI TANZANIA
Kifungu Na.
39.-(1) Mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano
(a) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anamuua au
anajaribu kumuua Rais; au
(b) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano anaanzisha vita dhidi
ya Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.
(2) Mtu yeyote ambaye, yumo katika ndani ya Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo yafuatayo, yaani-
(a) kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia, Rais;
(b) kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(c) kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au
(d) kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,na kubainisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi or machapisho au kwa kitendo chochote cha siri kinachojionyesha cha hali yoyote, atakuwa na hatia ya kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifo.
(3) Mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya
Muungano–
(a) aliye na mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko;
(b) anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au
(c) anabeba silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia, kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.
(4) Mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kwa nia ya kumsaidia adui wa Jamhuri ya Muungano anafanya kitendo chochote kinacholenga au kinachoweza kutoa msaada kwa adui huyo, au kuingilia kwa maelekezo Serikali ya Jamhuri ya Muungano, au kuzuia operesheni ya Majeshi ya Ulinzi au Jeshi la Polisi, au kuhatarisha maisha, ana hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo
Itapendeza sana kama members wataisoma tu kwa ajili ya uelewa but without comment
Muwe na jioni njema