Tanzania na huku kwetu

KAKA A TAIFA

JF-Expert Member
Apr 27, 2011
566
80
Tofauti ya nyumba ya mlala hoi na mwenye nacho huku tukisema maisha bora kwa kila mtanzania?kweli au kiini macho?
 
Attachments

  • DSC04040[1].JPG
    DSC04040[1].JPG
    28.7 KB · Views: 183
  • DSC04038[1].JPG
    DSC04038[1].JPG
    19.2 KB · Views: 188
  • DSC04035[1].JPG
    DSC04035[1].JPG
    21.1 KB · Views: 162
  • uchumi umekuwa.jpg
    uchumi umekuwa.jpg
    55.5 KB · Views: 142
Hayo ni madaraja mbalimbali ya wananchi wa tanzania, kuna matajiri, masikini, kwa kuangalia hizo picha hapo, nakubaliana na wewe kwamba pote ni kwetu tanzania, maisha mijini na vijijini ni tofauti, katika nchi yetu serikali haijengi nyumba za kutosha kwa ajili ya watu wake, tanzania wengi hujenga nyumba zao wenyewe hata kwenye majiji makubwa, makazi yasiyo na mpangilio ni proof kwa hilo, hizo nyumba hapo juu ingelikua serikali imejengea watu wa mjini tuu na kuwaacha wa vijijini kama zilivyo hizo nyumba ningesikitika sana. Lakini huwezi kulaumu kwa nini huyo anakaa nyumba nzuri wakati wengine wanakaa nyumba za kama hizo ambazo hazistahili hata jina la nyumba, kila mtanzania ana njia yake ya kupata hela, yaani kama unaendesha gari, kuna wengine wanavunja sheria na kuendesha kwa kasi, pamoja na kupenda shtikati(wala rushwa na mafisadi) kunawengine wanaendesha kwa usalama na wanafuata njia zote, hapo lazima pawe na tofauti kama unavyoona kwenye makazi hayo hapo juu
 
Nisingependa kujudge watu nisiowafahamu....kwa hiyo siwezi kusema hao wenye nyumba nzuri wamezipataje na hao wenye nyumba za udongo wamezipataje.

Ila kama general rule: Maisha bora kwa kila mtanzania, maana yake sio kila mtu atapata vya bure. Kama unaamka asubuhi na kwenda kufanya kazi kwa bidii mpaka jioni (na hapa inategemea na kazi), then utegemee kupata nyumba nzuri.....ila kama wewe siku nzima unapiga pombe tu, na longolongo...au unafanya kazi isiyolipa, then usitegemee kupata nyumba nzuri.

Huwezi kuamka asubuhi tu ukaanza kugawa nyumba za bure?.....atazijenga nani? kwa hela za nani?
 
Halafu cha kushangaza kama si kusikitisha wote utakuta ni wakereketwa wa jembe na nyundo.
 
Hao ndio wenyewe wanaombiwa maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana. Hivyo bado wanasubiri hayo maisha bora.<!-- google_ad_section_end -->
 
Hapo ndo hutaamini...tena hawa ndo wanaangusha wapigania haki za wananchi wakilanda mitaani na kusema CCM oyee
 
Nisingependa kujudge watu nisiowafahamu....kwa hiyo siwezi kusema hao wenye nyumba nzuri wamezipataje na hao wenye nyumba za udongo wamezipataje.

Ila kama general rule: Maisha bora kwa kila mtanzania, maana yake sio kila mtu atapata vya bure. Kama unaamka asubuhi na kwenda kufanya kazi kwa bidii mpaka jioni (na hapa inategemea na kazi), then utegemee kupata nyumba nzuri.....ila kama wewe siku nzima unapiga pombe tu, na longolongo...au unafanya kazi isiyolipa, then usitegemee kupata nyumba nzuri.

Huwezi kuamka asubuhi tu ukaanza kugawa nyumba za bure?.....atazijenga nani? kwa hela za nani?
Mkuu, sasa mwalimu akiwa pale Kalya Kigoma, akiamka subuhi sana na kuwahi shuleni kufundisha wanafunzi kwa bidii sana, na kurudi kwenye nyumba yake ya nyasi aliyopangisha pale ndo kipato chake kitaongezeka na kuwa na uwezo wa kujenga kibanda cha vyumba viwili???

Issue sio kufanya kazi, issue ni kuwa kimjinimjini......maana yake ni kwamba, hata ukiwa Mwalimu Pale Kashagulu Kigoma, unaamka asubuhi sana, badala ya kwenda shuleni, unakwenda shambani kwako ulipolima karanga na alizeti, then ikifika saa tatu asubuhi ndo unaenda kufundisha.........That is what is called working hard kwa wafanyakazi wa serikali wa kada hiyo!!

Hawana Posho za kukalia ****** yao wala kufanya kazi kwa bidii kwa maana ya kula chaki kwa bidii hakuwaongezei hata penny.
 
mkuu, soma kipengele kwenye mabano.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom