Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 590
- 706
“Changamoto ya ajira nchini Tanzania haiko kwenye ukosefu wa kazi, bali kwenye mfumo wa unyonyaji unaoendelea, hususan katika sekta binafsi. Watu wanatumia muda wao mwingi, maarifa yao ya hali ya juu, na nguvu zao kuzalisha thamani kubwa kwa waajiri, lakini malipo wanayopata ni duni, yasiyolingana na juhudi zao. Wengine hulipwa kwa kuchelewa, wengine hawalipwi kabisa/wanadhulumiwa. Hili si tatizo la ajira, bali ni udhalilishaji wa nguvu kazi. Na hapo ndipo penye kiini cha changamoto. Na hiyo ndiyo chanzo kikubwa cha kukuza ukatili wa kijamii, kiuchumi na kisaikolojia.”-Alloyce, P.R.