Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,014
- 2,664
Wananchi wa Tanzania tunataka kuyasoma wenyewe hayo makaratasi ya makubaliano ya ubia na Barrick mliosaini kwa jina letu.
Taarifa rasmi ya Barrick inasema wao walivyokubaliana kuhusu mgao wa faida ni:
Economic benefits from Bulyanhulu, Buzwagi, and North Mara would be distributed on a 50/50 basis between the new operating company and the Government of Tanzania. The Government’s share of economic benefits would be delivered in the form of royalties, taxes, and a 16 percent free carry interest in the Tanzanian operations.
MAANA YAKE, pato la Tanzania la asimilia 50 litapatikana kwa kujumlisha kodi, mrabaha na ubia wetu wa 16%.
Waziri Kabudi, Rais Magufuli na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, wanasema hamsini yetu inakuja baada ya kuwa tushapata kodi, mrabaha na mgao wa ubia (16%), na hivyo tunapata zaidi hata ya mwekezaji (70% kwa maneno ya Kabudi).
Hizi taarifa zinapingana. Na tunasomewa tafsiri na kila upande, maandishi yenyewe hatuonyeshwi. Kwa nini?
Tunadai kuonyeshwa mkataba.