Tatizo wabongo tunalalamika saaaaaana, hatuchukui action. Watu ni waoga utadhani viumbe gani vile. Hakuna asiyejua chanzo cha matatizo haya, majority ya watanzania tunajua lakini, hatuko tayari kureact. Bongo zetu Watz sijui zikoje au MAGAMBA wametufanya mazuzu au?
Chukua mfano mrahisi wa kinachoendelea Igunga. Ni kweli CCM wana wakati Mgumu Igunga, lakini kama watanzania tngekuwa watu wa action, CCM wangekuwa wanahutubia uwanja mtupu. Watu wanajua Rostam kajiuzulu kwa kashfa ya ufisadi, alafu Rostam huyo huyo anakwenda kuombea kura mgombea wa CCM. Pili, nirudi kwenye hoja ya ajali.
Dereva analewa na unamwona kabisa kalewa, anakimbiza gari kama kichaa, alafu abiria wanacheka na kuanza kusema kuwa "leo tutawahi kufika!!" kumbe anawahi kwenda kuzimu. Ajali ikitokea anaanza kulalamika anasahau kuwa alikuwa anazungumzia kuwahi. Tuna akili za mbayuwayu, mii nashangaa watu tunamsema JK mbayuwayu lakini na sisi wenyewe mbayuwayu tuu.
Hoja yangu ya msingi, tushikamane na lets take action in Unity.
Kuna siku nilikuwa kwenye gari kukawa na mjadala wa masuala ya siasa. Tulipoanza kuzungumza nikawa nazungumzia uovu uliopo serikalini, watu wananikodolea macho na mmoja akaniambia, "broo vipi unazungumza hivi huogopi?".
Nikamjibu kuwa mimi nakuogopa wewe ambaye unaogopa kusema ukweli. Siwaogopi waovu ambao wanatengeneza vitambi kwa kula jasho letu.