Ndumilakuwili
Member
- Aug 6, 2011
- 14
- 4
Ukiangalia ajali kubwa kubwa zilizowahi kutokea nchi hii, ni kutokana na uzembe wa wahusika na pengine serikali kwa sehemu kubwa. Zimekuwa zikitokea ajali zinazofanana fanana pasipo kupatiwa ufumbuzi. Hebu kumbuka miaka ya tisini mwishoni Treni ya reli ya kati ilianguka na kudidimia kwenye maji na kuua watu wengi sana, ikatokea nyingine inayofanana nayo mwaka 2002 kule Dodoma pia ikaua zaidi ya watu 200.
Vingunguti watu wengi walikufa kwa MABOMU kutokana na uzembe tu ambao walitakiwa warekebishe isitokee tena, lakini haikuwa hivyo, watu wengine wengi tena wakateketea Gongo la mboto kwa ajali ile ile ya mabomu. Haitoshi mwaka 1996 zaidi ya watu 1,000 waliteketea kwenye ajali ya Meli MV Bukoba Kule Mwanza, hatua hazikuchukuliwa kudhibiti.
Mwaka huu tena kosa lile lile la kujaza uzito zaidi likasababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 kwenye meli ya Islander kule Zenji, Ukija Upande wa barabarani huko ndio "BUCHANI" watu tunateketea serilkali inasubiri kuunda tume za kuchunguza vifo vyetu kila siku, huku wakila maposho yasiyo na idadi.
Hii imekaa vipi waungwana?