Tanzania na ajali zinazofanana fanana!

Ndumilakuwili

Member
Aug 6, 2011
14
4
Ukiangalia ajali kubwa kubwa zilizowahi kutokea nchi hii, ni kutokana na uzembe wa wahusika na pengine serikali kwa sehemu kubwa. Zimekuwa zikitokea ajali zinazofanana fanana pasipo kupatiwa ufumbuzi. Hebu kumbuka miaka ya tisini mwishoni Treni ya reli ya kati ilianguka na kudidimia kwenye maji na kuua watu wengi sana, ikatokea nyingine inayofanana nayo mwaka 2002 kule Dodoma pia ikaua zaidi ya watu 200.

Vingunguti watu wengi walikufa kwa MABOMU kutokana na uzembe tu ambao walitakiwa warekebishe isitokee tena, lakini haikuwa hivyo, watu wengine wengi tena wakateketea Gongo la mboto kwa ajali ile ile ya mabomu. Haitoshi mwaka 1996 zaidi ya watu 1,000 waliteketea kwenye ajali ya Meli MV Bukoba Kule Mwanza, hatua hazikuchukuliwa kudhibiti.

Mwaka huu tena kosa lile lile la kujaza uzito zaidi likasababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 kwenye meli ya Islander kule Zenji, Ukija Upande wa barabarani huko ndio "BUCHANI" watu tunateketea serilkali inasubiri kuunda tume za kuchunguza vifo vyetu kila siku, huku wakila maposho yasiyo na idadi.

Hii imekaa vipi waungwana?
 

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
513
147
Tatizo wabongo tunalalamika saaaaaana, hatuchukui action. Watu ni waoga utadhani viumbe gani vile. Hakuna asiyejua chanzo cha matatizo haya, majority ya watanzania tunajua lakini, hatuko tayari kureact. Bongo zetu Watz sijui zikoje au MAGAMBA wametufanya mazuzu au?

Chukua mfano mrahisi wa kinachoendelea Igunga. Ni kweli CCM wana wakati Mgumu Igunga, lakini kama watanzania tngekuwa watu wa action, CCM wangekuwa wanahutubia uwanja mtupu. Watu wanajua Rostam kajiuzulu kwa kashfa ya ufisadi, alafu Rostam huyo huyo anakwenda kuombea kura mgombea wa CCM. Pili, nirudi kwenye hoja ya ajali.

Dereva analewa na unamwona kabisa kalewa, anakimbiza gari kama kichaa, alafu abiria wanacheka na kuanza kusema kuwa "leo tutawahi kufika!!" kumbe anawahi kwenda kuzimu. Ajali ikitokea anaanza kulalamika anasahau kuwa alikuwa anazungumzia kuwahi. Tuna akili za mbayuwayu, mii nashangaa watu tunamsema JK mbayuwayu lakini na sisi wenyewe mbayuwayu tuu.

Hoja yangu ya msingi, tushikamane na lets take action in Unity.

Kuna siku nilikuwa kwenye gari kukawa na mjadala wa masuala ya siasa. Tulipoanza kuzungumza nikawa nazungumzia uovu uliopo serikalini, watu wananikodolea macho na mmoja akaniambia, "broo vipi unazungumza hivi huogopi?".

Nikamjibu kuwa mimi nakuogopa wewe ambaye unaogopa kusema ukweli. Siwaogopi waovu ambao wanatengeneza vitambi kwa kula jasho letu.
 

Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,482
564
MKUU umenena kweli pia AJALI za moto ktk masoko ya Mbeya
  1. Mwaka 2006 moto uliwaka soko la Mwanjelwa magari ya zima moto yalinza kuprove failure kabisa wengi waliuanza umaskini hapohapo
  2. Mwaka 2010 soko la uhindini liliungua kwa moto sehemu ambayo ni karibu kabisa na kituo cha zima moto lakini waliendelea kuprove failure
  3. Jana 2011 saa 3 asubuhi moto ulizuka Soko la SIDO ambalo walihamishiwa wafanya biashara walio unguliwa Mwanjelwa. Kama kawaida yao zima moto walifail hadi kusababisha RAIA kuwarushia mawe polisi waliingilia nao wakapigwa mawe na wananchi maana wlikuja wakiwa too late

Ajabu sisi WATZ hatujifunzi kutokana na makosa yaliyo fanyika jana kimsingi hali ni MBAYA
 

Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
11,474
6,019
Wa-Tz wengi ni:- waoga, wavivu, waongo, wazembe, wanafiki, wenye vichwa vizito kuamua,.....nk, nk. Ova!
 

Yakuonea

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
602
265
Inaonyesha ni jinsi gani tulivyo mambumbumbu na hatujifunzi lolote kutokana na ajali / majanga yaliyowahi kutufika, usishangae ndugu yangu kwa kuwa hatuonyeshi kwa dhati kukabiliana na majanga haya basi yataendelea tu kujirudia, nchi inakabiliwa na majanga na siku zote hatuko tayari, hatuna vifaa ya uokoaji na wala hakuna uwajibikaji wowote, huu ni ubabaishaji
 

kaly

Member
Aug 6, 2011
63
3
Mimi binafsi naumia sana kuskia kila ukikucha majanga na yanoyoyakana na uzembe hivi mamlaka huska hazijifunzi kutokana n makosa yanatokea?. Hakika imefika muda tubadili huu mfumo wa uongozi ili tuishi kwa amani.Hawa magamba wameshaonekana wameshindwa na kwa nn tuendelee kuongozwa na watu wanaotuua bila hatia?. Vijana tuamke
 

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Tz tumekalia kudhibitiana tu. Mbeya Mwakipesile kakaa pale akifikiria kuwadhibiti tu rivals waJk na ccm kiujumla wake, hakukuwa na mikakati ya namna ya kukabiliana na majanga kama haya ambayo yalishatokea former Mwanjelwa market
 

Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,202
815
Hiyo kesi ya waliokamatwa kwa uzembe wa kuzama kwa meli ni ya kisanii tu kuwapunguzia wananchi jazba wasije wakaiadhibu serikali kwa uzembe. Itaendelea kwa miaka 3 au 4 kisha kama kawaida wataachiwa huru. Serikali itasema "Tumejifunza kwa tukio hilo' sasa hivi tuko makini sana. Mwisho wa mchezo.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom