Kauli ya kuita watu mikenya ni kukosa nidhamu katika mjadala kama huu. Kila mtu ana haki ya kujieleza lakini usimuumbue mwenzako. Ameuliza swali na ungempa tu jibu ingefaa zaidi. Na sisi ni Wafrika mipaka yetu hatukuiamua, hatukushirikishwa wala kushauriwa Mwalimu baba wa taifa alikiri hili katika mojawapo ya hotuba zake. Ila tujiulize maswali nchi yetu imefikia kiwango cha kujitia viwanda. Miundo mbinu bado haikidhi mahitaji ya kimsingi usizungumzie viwanda. Mwanauchumi kwa jina la W.W Rostow aliorodhesha hatua za nchi kukua na katika hatua hizo tuko mbali sana na kilele chake. Ukipata nafasi ya kusafiri nchi nyingi utagundua kwamba mifumo yetu bado iko katika karne ya 20 ingawa tunatumia TEHAMA ya karne ya 21. Watu wengi hawapendi kujituma wanapenda kuwe na nyapara ndio wafanye kazi.... Tubadilishe mtazamo na mielekeo nchi itakuwa na uchumi utastawi