Tanzania mbioni kuanza kutengeneza magari

Tanzania mbioni kuanza kutengeneza magari

Bikomabilioni

Member
Joined
Nov 10, 2018
Posts
46
Reaction score
33
 Kampuni ya Bosch kutoka Ujerumani inayojihusisha na masuala ya Teknolojia imeonesha nia ya kuwekeza nchini katika masuala ya ufumbuzi/kukuza Teknolojia kutokana na nchi kuwa fursa kubwa ya ukuaji wa teknolojia ikiwa pamoja na kuanzisha kiwanda cha kuunganisha vipuli vya magari (automotive assembly)

 kampuni ima lengo la kuwashirikisha washirika wa ndani katika kutekeleza mipango yao, ambayo ni pamoja na kuwapa ujuzi na kufanya kazi na Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kuwapa mafunzo ya kiufundi kwa kutumia teknolojia watazozileta. Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza kufanya kazi na vituo 50 vya kutengeneza magari nchini kwa kuwapa haki ya kutumia jina la kampuni hiyo pamoja na mifumo ya kuzalisha na kuuza bidhaa nzuri kulingana na ubora husika, amabapo kila kituo kitapewa Euro 300,000 na kila kituo kitachangia kitakachoshriki kitachangia Euro 10,000

 katika mipango yao ya muda mrefu baada ya kufanya uchunguzi watawekeza katika viwanda vya kutengeneza magari. Kulingana na utafiti wao, kanda ya Afrika Mashariki ina soko lenye uhitaji wa magari kati ya 600,000 na 1,000,000.

 Aidha Bosch imewekeza katika nchi 13 za Afrika na Tanzania ndiyo target yao kwa sasa.
 
Kwa mazingira haya ya jiwe ya kukurupuka lazima mwekezaji akimbie kabla hajafikia makubaliano.

Kama tupo karne hii na umeme unakatika hata siku nzima ni ajabu sana hii nchi nibora ningezamia kule kule mbele.
 
Kwanza wameshapewa masharti ya kuachana na ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme mbuga ya Seoul
 
Kwanza wameshapewa masharti ya kuachana na ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme mbuga ya Seoul
Mazingira ya sasa ya hapa sio favourable kwa investors. Wanaweza waka spot potential ila wakifanya feasibility study wanakimbia bila taarifa.
 
Mazingira ya sasa ya hapa sio favourable kwa investors. Wanaweza waka spot potential ila wakifanya feasibility study wanakimbia bila taarifa.
Mkuu akikosa change kwenye bakuli anaweza kuwaambia walipe kodi ya miaka mitano mbele.

Katiba ni mbovu sana, anachosema rais ni final say.
 
magari tunatengeneza muda mrefu tu...tena ya kuvutwa na wanyama au kusukumwa.
 
Kwa mazingira haya ya jiwe ya kukurupuka lazima mwekezaji akimbie kabla hajafikia makubaliano.

Kama tupo karne hii na umeme unakatika hata siku nzima ni ajabu sana hii nchi nibora ningezamia kule kule mbele.
SI USEME TU NI BORA UNGEKUWA NGURUWE TU ULAYA?

MAANA KILA KITU NI SIASA TU KWENU HALA! [emoji57]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani tangu awali magari yetu yalikuwa yanatengenezwa wapi? Tuna garage kibao hadi vichochoroni. Nimeisoma hii habari hakuna sehemu yoyote iliposema wataunda Magari sasa unashabikia nini? Kutengeneza hata mimi natengeneza.
 
Kichwa cha habari kinasema "kutengeneza magari" ila maelezo yanasema "kuunganisha vipuri" yaani car assembly.

Kuna tofauti kati ya kutengeneza, kuunda, na kuunganisha. Wewe unataka kumaanisha nini?
 
Back
Top Bottom