Tanzania mbioni kuanza kutengeneza magari

Tanzania mbioni kuanza kutengeneza magari

Kwa mazingira haya ya jiwe ya kukurupuka lazima mwekezaji akimbie kabla hajafikia makubaliano.


Kama tupo karne hii na umeme unakatika hata siku nzima ni ajabu sana hii nchi nibora ningezamia kule kule mbele.
Hatari tupu Bado hujakutana na Dudu linaloitwa Nemc jingine OSha jingine Maafisa Afya jingine zima moto bora ata hill la zima moto, Bado Sana hatuja jianda kwenye uwekezaji wa viwanda!!
 
 Kampuni ya Bosch kutoka Ujerumani inayojihusisha na masuala ya Teknolojia imeonesha nia ya kuwekeza nchini katika masuala ya ufumbuzi/kukuza Teknolojia kutokana na nchi kuwa fursa kubwa ya ukuaji wa teknolojia ikiwa pamoja na kuanzisha kiwanda cha kuunganisha vipuli vya magari (automotive assembly)

 kampuni ima lengo la kuwashirikisha washirika wa ndani katika kutekeleza mipango yao, ambayo ni pamoja na kuwapa ujuzi na kufanya kazi na Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kuwapa mafunzo ya kiufundi kwa kutumia teknolojia watazozileta. Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza kufanya kazi na vituo 50 vya kutengeneza magari nchini kwa kuwapa haki ya kutumia jina la kampuni hiyo pamoja na mifumo ya kuzalisha na kuuza bidhaa nzuri kulingana na ubora husika, amabapo kila kituo kitapewa Euro 300,000 na kila kituo kitachangia kitakachoshriki kitachangia Euro 10,000

 katika mipango yao ya muda mrefu baada ya kufanya uchunguzi watawekeza katika viwanda vya kutengeneza magari. Kulingana na utafiti wao, kanda ya Afrika Mashariki ina soko lenye uhitaji wa magari kati ya 600,000 na 1,000,000.

 Aidha Bosch imewekeza katika nchi 13 za Afrika na Tanzania ndiyo target yao kwa sasa.
kabla hujatuaminisha andiko lako ,hebu tuangalie nchini mwetu ni magari gani hasa yanayotumika,90% ni magari ya kijapan,ndio yenye soko,sasa hivo vikobe vya kijerumani utamuuzia nani,sisi uwezo wetu ni mitumba ya kijapani
 
Kila mwaka tunaambiwa tuko mbioni kutengeneza magari na mpaka leo hatuyaoni magari hayo. Ooh mara toyota wanaanzisha kiwanda hapa, Ooh mara kampuni ya magari ya Foton wanafungua kiwanda, leo Ooh kampuni ya bosch ya ujerumani inaanzisha kiwanda. Inaonekana hizi mbio hazina mwisho. Tusishangae tukazisikia hadithi hizi kwa karne kadhaa zijazo, Sasa tunasubiri kuleta hadithi kuhusu kampuni ya volvo kujenga kiwanda hapa. Maneno meeeeeeengi, utendaji sifuri.
 
Safi waje tu, wamenusa stiglers gorge itatoa fursa umeme wa bei rahisi. Mpaka mradi unakamilika nao watakuwa na nguvu kazi yenye taalum inayohitajika
 
Eti kuonesha nia!! Hopeless

Kwa uchafu uliopo katika awamu hii, kila kitu kitaishia kwenye, 'kuonesha nia'. Narudia tena, mimi nimewahi kushiriki kwenye ranking za kuongoza uwekezaji duniani.

Ukweli ni kuwa hakuna mwekezaji makini anayeweza kuwekeza kwenye nchi ambayo demokrasia ni duni, utawala wa sheria haupo, hakuna utawala wa kitaasisi.

Tutapata wachuuzi lakini siyo wawekezaji.

Mahali popote pasipo na demokrasia au utawala wa sheria ni risk area kwa sababu kwa hulka ya binadamu, hataki kubanwa. Kwa hiyo hata pakiwa na utulivu leo, siku yoyote panaweza kupasuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom