Tanzania kwa sifa...!

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Kumekuwa na kasumba hapa nchini kwetu ya kuwakaribisha kwa bashasha esp kwa watu walioweza kufanya mambo fulani makubwa. Hilo sikatai lakini jeh, kuna haja ya kufanya zaidi ya hapo? Kwa mfano, hivi majuzi Hashim Thabeet (kijana aliyetumia juhudi zake binafsi kufika hapo alipofika), alirudi nchini na kupokelewa na viongozi wa serikali na si kwamba hiyo ilitosha bali pia alipata fursa ya kukaribishwa ikulu. Lakini je! Na wale wasiojiweza kama vile ombaomba, wajane, watoto wa mitaani n.k walishawahi fanyiwa hivyo?. Ikumbukwe hawa Wako hapa hapa nchini….!

Nani wakuangaliwa zaidi? Waliofanikiwa tayari, au hawa waliochini? NISAIDIENI WADAU…
 
Si Watanzania tu, hataThomas Campbell alisema "Victory has a thousand fathers, defeat is an orphan"

Sasa hata aliyecheza naye kidali atasema alichangia mafanikio yake, maana walikimbizana. Kilichobaki wewe fanya unachoweza kutuonyesha tofauti.
 
Ni kweli watz tunashabiki sana na watu waliofanikiwa.nilifurahi huyo jamaa aliwaambia hakuna atakayejisia kwamba kamsaidia kufika hapo alipo. Sijui hata hao viongozi wa serikali hilo fungu la mapokezi walilitoa wapi.kingine ni kwamba wengine hufikiria wakiwa karibu na mtu kama huyo anaweza kupata lambalamba.Namsifu mengi kwakuwa hujishugulisha na wanyonge.matajiri wengine wao kazi ni kuchangia vyama.uchaguzi wa vijana mtu katoa 400ml.uchaguzi mkuu unategemea atatoa ngapi?na nani atamlipa?samahani kama nimechanganya mambo,vitu vingine vinatia hasira.
 
Back
Top Bottom