Tanzania kuwa sehemu ya uchimbaji wa mafuta nchini Uganda, kupata hisa za asilimia 8

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Pamoja na Tanzania kufaidika kiuchumi kutokana na ujenzi wa bomba la Mafuta toka Kabaale, Uganda hadi jijini Tanga, bado itapata hisa za asilimia 8 katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji mafuta..

Mradi huo wa bomba la mafuta ambao una urefu wa kilomita 1,445 ambao umeanza kujengwa umetajwa kuwa na manufaa kwa pande zote mbili ikizingatiwa kuwa mafuta hayo yatasafirishwa kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga kabla ya kuuzwa katika nchi nyingine.

Kulingana na Jarida la The Guardian linaeleza kuwa uchimbaji wa mafuta katika mji wa Kabaale uliopo Wilaya ya Hoima unatarajiwa kuanza 2018 baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa bomba hilo ambalo litagharimu Dola za Marekani bilioni 4 mpaka kukamilika kwake.

“Kenya imesema itachukua hisa za 2.5% za uchimbaji mafuta , Tanzania itachukua 8%. Mtambo wa kusafisha mafuta unatarajia kuanza 2018 na kuzalisha mapipa 60,000 ya mafuta kwa siku na Uganda itaanza kusafirisha mafuta mwaka 2020”, linaeleza jarida hilo.

Licha ya Tanzania kuwa sehemu ya wadau wa uzalishaji mafuta hayo ambayo yanapatikana katika Ziwa Albert nchi Uganda, itafaidika na ujenzi wa bomba la mafuta ambapo mradi huo utazalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira za muda mfupi 20,000.

Zaidi, soma hapa => Tanzania kupata hisa katika uchimbaji wa mafuta nchini Uganda | FikraPevu
 
Back
Top Bottom