Tanzania kuwa kama Singapore, China, Japan, Korea, Malaysia inawezekana?

TPP

JF-Expert Member
Mar 18, 2023
650
782
Kutokana na utafiti wangu mdogo nilio ufanya katika nchi ya Tanzania nime gundua kitu kimoja

Raia wengi wa Tanzania wanapenda na wanataka nchi yao kuwa na maendeleo kama yalivyo mataifa haya:-
i, Singapore
ii, Malaysia
iii, Korea ( South & North )
iv, Japan
v, China( Hongkong, Macau, Taiwan, PRC )
vi, Vietnam

Ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo mapya ya kasi ya kiuchumi ya haya mataifa yameanza miaka ambayo haitofautiani sana na Tanganyika kuwa huru pamoja na muungano wa nchi mbili na kuwa nchi moja Tanzania

Kiwastani maendeleo ya kasi ya kiuchumi ya hizi nchi ni kati ya miaka ya 1950s, 1960s, hasa hasa miaka ya miaka ya 1970s- 1990s

Elimu ina mchango katika maendeleo ya haya mataifa lakini jambo la msingi sana ni "mfumo mzima wa malezi na maisha"

Mfumo wa malezi na maisha wa haya mataifa ulio changiwa kwa asilimia kubwa na falsafa ya "Confucianism" ndio msingi mkuu wa maendeleo ya kasi ya hizi jamii.

Ni rahisi sana nchi kuendelea kama mfumo wa malezi na maisha ya watu wake ni bora kazi ya serikali inakuwa katika mtiririko bora wa kuongoza, ubaya ni kuwa "mfumo wa maisha na malezi wa Watanzania ni mbovu haumuandai mtoto kuwa bora bali dhaifu kidunia".

Falsafa ya "Confucianism" imetawala sehemu kubwa ya East Asia kuanzia China kwenda Japan, Korea, Singapore, Malaysia, Vietnam n.k

Mwanafalsafa Confucius( Kong Qi/Fuzi) wa karne ya 5th-6th B.C.E kutoka China anaheshimika sana China na katika jamii za watu wa East Asia katika kushape societies zao
Confucius-Shanghai-China.jpg

Watawala waliopo na wanao waongoza Watanzania wanawakilisha mfumo mzima wa malezi na maisha ya Watanzania toka chini(utotoni) mpaka juu (ukubwani)

Kuna wanafalsafa wengi wa kale wamechangia jamii hizi za East Asians kuendelea mpaka hapo walipo Confucius ni moja wao.
 
Kama mkiacha wizi na rushwa na kujituma sana kwa kuuza bidhaa nje na kutengeneza vitu vya kwetu labda

Ila maisha yatabadilika baada ya kuuwa viongozi majizi na wengine wanaopokea rushwa kufungwa maisha na majina yakiwekwa hadharani

Tukikubali hayo basi tutafika
 
Mfumo wa Tz uliotulea wa ccm siyo rahisi kufika huko ... Inabidi ifanyike overhaul ya mfumo wa nchi hii. Hayo mataifa maadili ni kipaumbele kwao jumlisha hardworking. Huku kwetu tunaongozwa na kuabudu watawala na boot-licking za kutosha.. sidhani kama tunaweza kufikia huko
 
Kama mkiacha wizi na rushwa na kujituma sana kwa kuuza bidhaa nje na kutengeneza vitu vya kwetu labda

Ila maisha yatabadilika baada ya kuuwa viongozi majizi na wengine wanaopekea rushwa kufungwa maisha na majina yakiwekwa hadharani

Tukikubali hayo basi tutafika
Hivi vyote ulivyo andika vina tengenezwa toka chini(utotoni) kuja juu(ukubwani) kupitia mfumo mzima wa malezi na maisha

Katika nchi ya Tanzania hivi vyote vina sifiwa na wazazi kwenda kwa watoto wao wakati China, Vietnam, Singapore..... Vinapigwa vita katika malezi na serikali
 
Mfumo wa Tz uliotulea wa ccm siyo rahisi kufika huko ... Inabidi ifanyike overhaul ya mfumo wa nchi hii. Hayo mataifa maadili ni kipaumbele kwao jumlisha hardworking. Huku kwetu tunaongozwa na kuabudu watawala na boot-licking za kutosha.. sidhani kama tunaweza kufikia huko
Upo sahihi. Mfumo wa maisha na malezi ndio unao amua maendeleo ya kasi ya taifa wakati huo Tanzania hakuna mfumo bora
 
Kutokana na utafiti wangu mdogo nilio ufanya katika hii nchi ya Tanzania nimengundua kitu kimoja

Raia wengi wa Tanzania wanapenda na wanataka nchi yao kuwa na maendeleo kama yalivyo mataifa haya:-
i, Singapore
ii, Malaysia
iii, Korea ( South & North )
iv, Japan
v, China( Hongkong, Macau, Taiwan, PRC )
vi, Vietnam

Ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo mapya ya kasi ya kiuchumi ya haya mataifa yameanza miaka ambayo haitofautiani sana na Tanganyika kuwa huru pamoja na muungano wa nchi mbili na kuwa nchi moja Tanzania

Kiwastani maendeleo ya kasi ya kiuchumi ya hizi nchi ni kati ya miaka ya 1950s, 1960s, hasa hasa miaka ya miaka ya 1970s- 1990s

Elimu ina mchango katika maendeleo ya haya mataifa lakini jambo la msingi sana ni "mfumo mzima wa malezi na maisha"

Mfumo wa malezi na maisha wa haya mataifa ulio changiwa kwa asilimia kubwa na falsafa ya "Confucianism" ndio msingi mkuu wa maendeleo ya kasi ya hizi jamii.

Mfano
Ni rahisi ukichukua jamii ya Han Chinese kutoka China na kuwaleta hapa Tanzania ndani ya miaka 30 Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kiuchumi Afrika na top ten duniani

Pia ukichukua Watanzania na kuwapeleka China ndani ya miaka hiyo hiyo 30 China itakuwa nchi yenye uchumi mbovu na mbaya Asia na duniani kiujumla.

Ni rahisi sana nchi kuendelea kama mfumo wa malezi na maisha ya watu wake ni bora kazi ya serikali inakuwa katika mtiririko bora wa kuongoza, ubaya ni kuwa "mfumo wa maisha na malezi wa Watanzania ni mbovu haumuandai mtoto kuwa bora bali dhaifu kidunia".

Falsafa ya "Confucianism" imetawala sehemu kubwa ya East Asia kuanzia China kwenda Japan, Korea, Singapore, Malaysia, Vietnam n.k

Mwanafalsafa Confucius( Kong Qi/Fuzi) wa karne ya 5th-6th B.C.E kutoka China anaheshimika sana China na katika jamii za watu wa East Asia katika kushape societies zaoView attachment 2600198

Watawala waliopo na wanao waongoza Watanzania wanawakilisha mfumo mzima wa malezi na maisha ya Watanzania toka chini(utotoni) mpaka juu (ukubwani)

Sio rahisi sana Watanzania kuendelea kama hawato changanywa au changamana na jamii zenye mfumo bora wa kimalezi na kimaisha.

Kuna wanafalsafa wengi wa kale wamechangia jamii hizi za East Asians kuendelea mpaka hapo wali Confucius ni moja wao.
adui wa watanzania ni ccm
 
  • Thanks
Reactions: TPP
Kwanza. Nadhani hizi nchi hazifanani zenyewe kwa zenyewe.

China haifanani wala haijwahi kufanana Japan kwa vingi. Hata sera, uongozi na tamaduni zao ni tofauti - historically na hata leo.
Singapore na Korea Kusini kiasi labda.
Point yangu ni hivi, unataka Tanzania iweje? Maana haiwezi kuwa kama Japan, China na S. Korea/Singapore maana hizo kila moja ni tofauti.
Yaani haiwezi kuwa kama Marekani, Hispania na Russia.

We need to choose the right model.
 
Unafahamu kuhusu usambaaji wa falsafa ya Confucianism na mchango wake East Asians?! hapa ndipo mada ilipojikita

Sijasema Tanzania wacopy East Asia bali Tanzania na Watanzania wanahitaji kubuni falsafa mpya ya kimalezi na kimaisha itakayo kuwa bora kwao na kizazi chao
 
Falsafa au mfumo wa kimalezi na kimaisha wa watu huwa haubuniwi bali unaibuka na kujiunda kutokana na mchanganyiko wa mambo mengi sana na kwa muda mrefu sana.
 
  • Thanks
Reactions: TPP
Upo sahihi. Mfumo wa maisha na malezi ndio unao amua maendeleo ya kasi ya taifa wakati huo Tanzania hakuna mfumo bora
Maendeleo huja kutokana na mambo mengi sana lakini la muhimu zaidi ni aina ya uongozi na siasa za nchi. Mfumo wa maisha na malezi sio muhimu sana katika maendeleo.
 
  • Thanks
Reactions: TPP
Hatuwezi endelea labda tununue management toka nje ya kutusimamia. Mfumo wetu umeshindwa, labda kama tusingedai UHURU tungekuwa na maendeleo.
Ufisadi, uzembe, rushwa, uvivu haviwezi malizwa na mfumo wetu tulio nao.
 
  • Thanks
Reactions: TPP
Falsafa au mfumo wa kimalezi na kimaisha wa watu huwa haubuniwi bali unaibuka na kujiunda kutokana na mchanganyiko wa mambo mengi sana na kwa muda mrefu sana.
Pia unaweza kutengenezwa katika namna bora na jamii nzima ikajifunza kama alivyo fanya Kong Fuzi na emperor aka urasimisha huo mfumo kwa taifa na jamii nzima
 
Back
Top Bottom