omujubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 4,325
- 2,498
Habari wanajamvi.
Katika pitapita zangu nimekutana na hili tangazo kutoka Jeshi la Ulinzi na Usalama Tanzania (TPDF) na limeniacha na maswali kadhaa. Naombeni mwenye fikira kama zangu aungane name au mwenye fikira tofauti atupe mwanga wa ni nini kinahusiana na tangazo hili.
1. Je yewezekana jeshi la polisi limeshindwa kazi?
2. Je, nchi inaweza kuingia katika hali ya hatari wakati wowote kuanzia sasa?
3. Je, yawezekana utawala wa demokrasia Tanzania umeshindwa?
4. Au tutegemea nini kama nchi!!
Kwa heshima na taadhima nawasilisha
na mimi naona kama kuna ujumbe uliokusudiwa bali tangazo la saba saba limetumika tu.JW walishaona hali inazidi kuwa tete!! EL mwaka huu atawatoa jasho CCM pamoja na serikali yao.
Najuaribu kuiangalia hiyo rangi nyekundu iliyotumika kama alert kwa msomaji.
Lakini ni kwa nini kama kweli wana nia nzuri wasiingilie masuala yanayoisumbua nchi kama ufisadi!? Au ndio wameanza na wale maofisa wa SUMA JKT waliopelekwa mahakamani juzi juzi!?