Tanzania kushindana na Kenya ni AIBU

Tanzania kushindana na Kenya ni AIBU

calmdowndear

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
605
Reaction score
275
Hivi kwa nini tusishindane na NIGERIA au SOUTH AFRICA?

Kenya sio size yetu kabisaaa kama tukiacha uswahili. As it is tushawashinda wa Kenya kwenye kila kitu kasoro Katiba tuu bas.

Nadhani we should aspire for bigger things na sio hizi longo longo za kushindana na Kenya.

Mnaonaje?
 
Wabongo bana, kwa akili yako unazania Kenya si lolote? Wakati Bongo tuko bise kuzungumzia kujitoa EAC kenya wako bise kupiga kazi, maendeleo sio kuwa na utajiri wa rasilimali. Holand wana tegemea Bandali na uwanja wa ndege pekee buy wako far. Na usidhanie hata huko SADC kuna cha maana cha Tanzania kufaidi. SADC wamemonopolise wa south hasa makaburu, na ile south inakimbizana na wakina brazili,india, Rusia na kazalika. Kenya wanatuzidi mengi pamoja kwamba tuna sijui madini, Shirika lao la Ndege wana safari hadi za Ulaya wakati sisi za ndani ya nchi hatuwezi, nenda kacheki UWanja wao wa Jomo Kenyata ulivyo bise tofauti na wa Bongo, hivyo ishu sio kuwa na sijui mali, Urusi angekuwa ndo namba one basi Duniani kwa sababu ana Gas ya kufa mtu, ana utajiri mkubwa sana wa misitu hass kule Siberia, wana madini ya chuma na kazalika.
 
nikusahihishe mkuu sisi hatushindani na kenya bali kenya wapo busy kushindana na kivuli chetu
 
Kenya ni nchi ndogo sana kwetu inatakiwa tuanze kufikiri nchi za second world sio hizi
 
kenya wanatupiga bakola kila nyanja.
Viwanda., bandari, airports, elimu, tanzania tukasome..juzi nilisikia mkuu wa kaya anasema kaya yake sasa inahitaji wanasayansi...kama mwanae nikajiuliza ni kweli ndo sasa katambua hili..?
 
Kenya ni nchi ndogo sana kwetu inatakiwa tuanze kufikiri nchi za second world sio hizi
Kufikilia nchi za dunia ya pili kivipi? Kimawazo au kivitendo? Sio rahisi kama unavyo fikiria mkuu, tumeua kila kitu, tumeua elimu, tumeua viwanda vyote, tutaweza vipi kushindana, au hiyo gas na mafuta ndo zinatupa kichwa? Mkuu kwa sasa nchi nyingi sana zimegundua mafuta na gas kiasi kwamba tuna muda mchache kabla haijawa ishu ya kawaida.

USA kiongozi wa matumizi makubwa kabisa ya nishati hasa gas na mafuta ataanza kuchimba gas yake na kumpiku Urusi kama kiongozi wa uzalishaji wa gas Duniani.

Mataifa kama Brazili ambao ndo wanakuja kwa kasi tiyari anachimba gasi na mafuta.
Tutaweza kushindana na Kenya kwa vitendo na sio kukaa kwenye keybord huku tukishindana kimawazo
 
kenya wanatupiga bakola kila nyanja.
Viwanda., bandari, airports, elimu, tanzania tukasome..juzi nilisikia mkuu wa kaya anasema kaya yake sasa inahitaji wanasayansi...kama mwanae nikajiuliza ni kweli ndo sasa katambua hili..?

Mkuu ukweli ndo huo wana tuzidi kila sehemu, ila sisi huku ni maneno na tukizani tunaweza shindana kipropaganxa wakati wenzetu wanafanya kwa vitendo
 
Yaan Tz na Kenya! Unajua hebu watu waache upumbavu hawa Wakenya wana njaa mbaya! Tz ishindane na watu ambao pia wanapanda basi la makabila karne ya 21? Hdili ni jambo la kipumbavu na hatari...
 
Tanzania ishindane na South Africa?!! Labda ccm iondoke madarakani. Vijumba vyenyewe bado vya nyasi nchi nzima!!
 
Kama ni mafuta wamegundua mengi tu maeneo ya Turkana. Wakianza kuchimba TZ itazidi kuachwa.
 
Hakuna viongozi wa kuifikisha Tanzania hata robo ya south afrika.
 
Hivi kwa nini tusishindane na NIGERIA au SOUTH AFRICA?

Kenya sio size yetu kabisaaa kama tukiacha uswahili. As it is tushawashinda wa Kenya kwenye kila kitu kasoro Katiba tuu bas.

Nadhani we should aspire for bigger things na sio hizi longo longo za kushindana na Kenya.

Mnaonaje?
Lini Tanzania ilianza mashindano na Kenya? Wewe mongiki uliyekodishwa kuja kuchoma shule zetu?
 
Back
Top Bottom