Tanzania kupiga vita vitu feki haiwezekani?

Full charge

JF-Expert Member
Mar 1, 2018
1,550
1,422
Tafadhali niende kwenye mada.

Hivi kwanini nchi yetu isizuie au kukataza uingizaji wa vitu feki kutoka mataifa mbali mbali?

Nimeandika hivi nikiwa na maana ya kwamba vitu hivi vinatugharimu sisi walaji wa chini mfano; uingizaji wa vifaa vya umeme feki vinasababisha nyumba nyingi kuungua.

Najua kuwa vitu halisi (original) ni gharama kidogo ila faida ni kubwa kuliko hasara ya feki. Natambua kuwa watu wengi hatuna elimu ya kutambua uhalisi wa vitu hivi ndiyo maana napenda kuishauri selikari ipige marufuku uingizwaji wa vitu hivi.

Njia rahisi inayoweza kutumiwa na selikari ni kuwaambia watengenezaji (hususani mchina) kwamba sisi nchi yetu siyo shimo la taka taka ivo basi wapunguze bei iwe standard ili kila mtu aweze kumdu na kununua. Mfano; simu, nguo, vifaa vya umeme nk.

Yawekwe masharti na msako mkali kwa wafanya biashara watakaokaidi,hii ni pamoja na kuharamisha bidhaa hizo ziwe kama bangi hapo itasaidi.

Selikari itoe elimu kwa wananchi juu ya fida za kununua vitu halisi,mfano: simu halisi inauzwa sh 50,0000 bandia yake 35000 hapo ukiangalia utaona kuwa sisi tukizoeshwa kununua tunaweza.

Kwanini kwao hawatumii huu uchafu wanaotuletea huku,hapa utagundua kuwa wanatucheka na kutudharau sana.Leo nchi yetu ina madini chaajabu tunavaa mavyuma eti ni mikufu+pete wakati ilitakiwa hivyo vitu hata tusiwe na shobo navyo.
 
Hivi vitu fake vinaudhi Sana. Sio vifaa vya umeme tu hadi mavazi. Hamna kitu kinanikera kama uko zako mjini kwenye mzunguko ukakutana na kiatu ukaona ni kizuri. Unatoa 30,000 au 40,000 kununua unaweza ukavaa Mara mbili tu au tatu unashangaa kinaanza kufumuka.
 
Back
Top Bottom