Tanzania Kuna vifaa vingi vinavoingia ambavyo vikitumika vibaya ni hatari

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,611
8,746
Siwezi shangaa kama ngorongoro ni kipande Cha nchi ndani ya nchi basi la bandari na Dp world linawezekana.

Tuje kwenye mada ambayo Leo imenifanya kueleza na kuwa fumbua wananchi wenzangu.

Wengi wetu tumekuwa wahanga wa kufunguliwa magari yetu kwa mawili waibe gari au waibe vitu na unajiuliza hata kioo wajavunja Wala kuharibu kitasa.

Kumekuwa na fasheni Kila mtu kutumia funguo ya kidigitali na mara nyingi wengi utumia za kichana.

Mfumo wa ufunguaji ni wa mawimbi na mfumo huu unaweza kuclone funguo nyengine.
Kifaa hiki kumekuwa kikitumika vibaya hata kutegea pindi mtu anapofungua gari kwa funguo ya mawimbi.
Vipo aina nyingi ukiwa ulaya unashauriwa Bora kufunga kwa funguo direct kama usalama wa funguo ni mdogo.

Software mbali mbali za Bure na kununua.nchi za wenzetu wapo makini sana na software ambazo zinaweza kuwa jasusi na taarifa za nchi na hata kudukua.ila utashangaa mpaka wizara nyeti nayo inatumia bila kuchunguzwa na kitengo maalumu.

Kifaa Cha kuzuia mawasilinao .kifaa hiki mnakiona kwenye gari la raisi ila sio kwa raisi tu unaweza kutumia kwa ajili kuzuia vifaa kama drone,bomu la mawasilinao,mawasilinao kwa ujumla.
Sasa ukute majambazi wamekuja kuiba wakiwasha eneo ilo kesho mtalalamika polisi walikuwa Hawa patikani kwenye mawasiliano.

CCTV camera aina mbali mbali usipo kuwa makini unaweza kujikuta unarekodiwa bila kufahamu kama balbu zenye kamera,chaji ya simu,mdori,peni na mengine.
Ni kitu kizuri ila imekuwa tabia ya kutumiwa katika faragha za wapenzi.

NFC tool hivi ni vifaa ambavyo utumiwa kwenye kutengeneza kadi na kucopy kard.

Wale tunapenda kutembea na kadi za benki au kadi za kufungulia milango mfano hotel au ofisi.

Kifaa hiki kinaweza kutumia vibaya kuchukua taarifa zako na kutumia hatakavyo .hakikisha kadi yako iwe kwenye pochi ambayo Ina protect NFC.

Nitaendelea
 
Back
Top Bottom