nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
[TABLE="width: 1013"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
na Tatu Mohamed
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD]SERIKALI imepanga kujenga miundombinu ya reli kutoka Tanzania hadi Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kupewa tuzo ya kutoa mchango mkubwa katika sekta ya reli.
Aliwataka Watanzania kutarajia makubwa kwenye usafiri wa reli kwa kuwa amejipanga kuboresha njia zilizopo na kujenga reli hiyo ya DRC, ili kurahisisha usafirishaji hususan wa mizigo.
Migongano iliyokuwepo katika sekta ya uchukuzi imefanyiwa kazi tutaleta injini mpya, treni za ghorofa zitakuwepo, lakini pia tunawaalika wafanyabiashara wakubwa kuleta treni zenye kiyoyozi ndani.
Huu utaratibu wa mtu kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma kwa siku mbili hadi tatu utakwisha, tunataka mtu anayekwenda Kigoma atumie masaa yasiyozidi manne, alisema Dk. Mwakyembe akieleza mikakati ya kuboresha reli nchini.
Awali Mkurugenzi wa Tanzania Mwandi, Teonas Aswile, aliyempa tuzo hiyo Dk. Mwakyembe, alisema mchakato wa kumpata mshindi wa tuzo hiyo ulizingatia masuala muhimu ikiwemo faida za kiuchumi kutokana na shughuli zake katika kuboresha reli.
Kwa mujibu wa Aswile pamoja na waziri huyo, wadau wengine wa reli walioshindanishwa ni Injinia Festo Mwanyika (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Huduma za Reli) na Linford Mboma kutoka Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA).
Tuzo hii ni baada ya mkutano wa kwanza wa wadau wa masuala ya reli Afrika Mashariki uliofanyika kuanzia Julai 3 hadi 5 mkoani Kigoma, wadau wa reli walitakiwa kuchagua jina moja, alisema.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]