hali ya kiuchumi ya Nchi yetu ya tanzania baada ya uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga ipo taabani na sababu kubwa ikiwa matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi huo; licha ya bajeti kupita hakuna ajira, gharama za maisha zimekuwa kubwa, wafanyakazi hawalipwi kwa wakati, hospitali hazina madawa, n.k. Hali hii inanifanya niamini kuwa kama kutakuwa na matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi mkuu wa October 2015 basi Novemba 2015 nchi itafilisika rasmi, sio mbali sana! naomba kuwasilisha
Una predict November 2015, mbali kote huko? Kutokana na serikali kuwa bankrupt,
inafikiria kutanganza min budget mwezi January 2012, ambapo kodi ya bidhaa mbalimbali
zitapindishwa kati ya 5%-10% ili kufidia nakishi ya serikali kutokana na mdororo wa kiuchumi,
kushuka kwa thamani ya shilingi, kufindia pengo la pesa kutoka kwa wahisani ambao wamegoma
kutoa kama walivyoahidi (Uingereza tayari imeshakata 32% ya misaada iliyoahidi kutoa kwenye budget
ya 2011/12). Na kama hatutaridhia kuruhusu ndoa za jinsia moja (eti haki za mashoga). Nchi za UE
zikiongozwa na UK zitatukatia misaad ya kimaendeleo.
Zitto aliwaambia angalau wakiondoa matumizi yasiyo ya lazima kama kufuta seatting allowance kwa
wafanyakazi waandamizi wa serikali wataokoa > Tshs bilioni 7, Lakini serikali ya magamba wakiongozwa na
Mkulo na Sitta wakambeza. sasa ndiyo tunaletewa tena min budget! Ngoja tukome Watanzania haya yote
tunajitakia wenyewe!
Leo 1/11 ni wafanyakazi tu wachache wa serikali wamepokea mishahara yao. Sijui bado wananegotiate kukopa NSSF
au PPF maana mishahara ya mwezi May 2011, walikopa NSSF.