Tanzania kinara kuuza ardhi kwa wageni!

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
659
Jarida la The African
Report, limefichua
dili la serikali la
kuimilikisha ardhi
yenye ukubwa wa
hekari zaidi ya 300,000 kwenye
Bonde la Mto Rufiji
lililoko mkoani
Pwani kwa kampuni
ya Muasia wa
Bangalore inayojulikana kama
Karutari Global. Jarida hilo limeripoti
kuwa mwekezaji
huyo anatarajiwa
kujipatia hekari hizo
iwapo mipango hiyo
inayojadiliwa itakwenda vizuri. Kadhalika jarida
linasema Tanzania
inaongoza barani
Afrika eneo la Kusini
mwa Jangwa Sahara
kwa kumilikisha kiasi kikubwa cha
ardhi yake kwa
wawekezaji wa
kigeni na kwamba
hadi sasa imetoa
hekari zaidi ya milioni moja za
maeneo yenye
rutuba kwa
wawekezaji wa nje. Habari za kuuza ardhi
ya Afrika
zimechapishwa
kwenye jarida hilo
toleo namba 41 la
Julai 2012, lenye kichwa cha habari
toleo maalumu
“Namna wanasiasa
walivyoachia Dola
bilioni 100 za ardhi.
Taarifa maalumu ya uchunguzi wa siri ya
dili anayotishia
mamilioni ya
wakulima wa
Afrika.” Ripoti maalumu
iliyochapishwa
kurasa za 23 na 24 za
jarida hilo inaitaja
Tanzania kuwa
imeuza hekari 1,083,000 za ardhi
kuanzia mwaka
2006 na kuanika
kuwa watuhumiwa
wa ufisadi huo wa
ardhi ni wanasiasa na viongozi wa serikali
ambao hugawa ardhi
ya taifa kwa wageni
kwa kuingia ubia na
wageni . “Wakati mwingine
wanajichukulia ardhi
bila kufuata taratibu
na sheria zilizopo.
Huwahonga viongozi
wa vijiji na kuwashinikiza
kuitisha mikutano ya
haraka
inayowezesha
kutimiza azma hizo,”
jarida hilo likimkariri Barnaba Baha wa
asasi ya kimataifa ya
Action Aid. Ripoti inasema
kwenye bonde la
Mto Rufiji mpango
wa kuuza zaidi ya
hekari 300,000
unaendelea na kuitaja kampuni ya
India ya Karutari
Global iliyowekeza
nchini Ethiopia kuwa
ndiyo
inayokusudiwa kupewa eneo hilo. Jarida linaeleza
kuwa Karutari Global
ni kampuni ya
Bangalore
inayomilikiwa na
Muasia Sai Ramakrishna Karutari
aliyeelezwa kuwa ni
mmiliki wa majumba
ya kuendesha kilimo
(green house)
yanayozalisha miche zaidi ya milioni 650
za maua ya rozi kila
mwaka . Jarida linawakariri
wasemaji wa Benki
ya Dunia (WB)
wakishangaa uuzaji
huo wa ardhi kwa
kile wanachokiita ni dili dhidi ya maili za
mraba milioni 1.5 za
ardhi ambazo
hazijaguswa lakini
sasa zinatolewa kwa
wawekezaji wa kigeni na tawala za
Kiafrika. Watafiti wanaeleza
kuwa uporaji huu
wa ardhi ni aina
nyingine ya
kugombea Afrika
kama ule uliofanyika mwaka 1885 baada
ya mkutano wa
Berlin ulioigawa
Afrika kwa wakoloni
ambapo Tanganyika
( sasa Tanzania ) ilichukuliwa na
Wajerumani. Mtafiti kutoka
Ethiopia
akizungumzia kiama
cha wakulima wa
Afrika alikaririwa na
jarida hilo: “Ninasema
kinachotokea barani
Afrika ni kuigombea
Afrika lakini kwa hili
la sasa ni serikali
zenyewe kupora ardhi za watu wake
na kuwazawadia
wawekezaji.” Kama kawaida jarida
hilo linaeleza kuwa
viongozi wa Afrika
wameendelea
kuimbiwa nyimbo za
hadaa kuwa uwekezaji utaleta
ajira kwa vijana,
utaboresha
teknolojia ya kilimo
na kuongeza
uzalishaji utaokaopunguza
umaskini. Habari hizo zinaitaja
Tanzania, Kenya,
Zambia, Uganda,
Kongo , Ethiopia,
Mali, Msumbiji na
Liberia kuwa zinaonyesha sura ya
serikali za Afrika
zinavyojizatiti
kuvutia mitaji ya nje
kwenye sekta ya
kilimo. Hata hivyo jarida
linaeleza kuwa cha
kushangaza mipango
ya kujitwalia ardhi
za wakulima
pembezoni hufanywa kwenye
miji mikuu bila
kuwashirikisha
wakulima wamiliki
ambao ndiyo
wahanga wa uporaji huo. CHANZO: NIPASHE
JUMAPILI.
 
Back
Top Bottom