Muda wote mchana umeme haukuwepo mtaani kwetu, umeme umerudishwa kama saa 12 jioni, lakini kutoka saa 12 mpaka saa 2 usiku umeme umekatwa na kurudishwa zaidi ya mara kumi, tumelazimika kuzima kwanza vifaa vya umeme kwakuwa vikiunguwa Tanesco hawatalipa, lakini mbaya zaidi ni kuwa mgawo umeongezeka mara dufu, zamani siku za jpili ilikuwa si rahisi mtaani kwetu tukose umeme, siku hizi wanakata mpaka jpili. Ni vigumu kuzungumzia tatizo la umeme nchini, mi nafikiri vyombo vyote vya habari vingeandika habari moja tu ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho kuhusu umeme tu.
Inasikitisha na kustaajabisha kuwa mali zote hizi ilizojaaliwa Tanzania bado nchi haina hata umeme!. Nimefikiria kuwa pengine wazungu wanapotuzomea kuwa sisi ni nyani huwa hawakosei kwa kuwa maisha tunayoishi ni nyani tu ndo walipaswa kuishi hivi na si binadamu. Madini ya kila aina na ya thamani, maji ya mito, maziwa, mabwawa, bahari, milima, ardhi nzuri, misitu, mbuga za wanyama, bandari; lakini bado Tanzania haina umeme!
Wakati ule bajeti ya wizara ya nishati na madini ilipokataliwa na kutakiwa kuandaliwa upya umeme haukukatwa hata mara kama wiki 2 hivi, niliwaambia majirani kuwa subirini bajeti ipite mgawo zaidi ya uliopita, na ndicho kilichotokea!!
Aibu TANZANIA HAINA UMEME. Mi nipo tayari UFISADI uendelee lakini watuachie UMEME kwakuwa kunapokuwa na umeme wauza juisi na vinyoozi wa saluni tunapata hela ya kununua dagaa, tunapoendelea kukosa dagaa sababu ya umeme mwisho itabidi tufe.