Tanzania kiboko! Wote tuko Igunga, nchi iko gizani, bei ya bidhaa juu, shilingi inaporomoka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kiboko! Wote tuko Igunga, nchi iko gizani, bei ya bidhaa juu, shilingi inaporomoka!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by abduel paul, Sep 29, 2011.

 1. a

  abduel paul Senior Member

  #1
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wingi wa matukio TZ unaifanya Tz kutokuweka vipaumbele kwenye mambo ya msingi, yapata miezi kadhaa baada ya kauli za dharula kutolewa zikilenga utatuzi wa tatizo la umeme miezi inazidi kusonga tatizo la umeme halina unafuu, na hapa ndo dharula, Je isiyo dharula ikoje? Hivi ni kweli la Igunga ni muhimu kuliko matatizo mengine ya Tz? Ukizingatia baada ya uchaguzi atapatikana mbunge mmoja tu!?
   
 2. a

  abduel paul Senior Member

  #2
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi waTZ wote ni Wanasiasa???
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  nasikia lgunga hakuna mgao hata Tabora watu wanakenua meno eti serikali inafanya kazi wakishinda magamba wasitulalamikie vinyozi,mahospitalini, mafundi kuchomelea n.k oh umeme wa mgao oh umeme wanakata watajiju wapiga kura.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inamaana ccm kwenye kampeni igunga wanasema je kuhusu umeme, kupanda kwa bei ya vitu pamoja na ufisadi? Kwani kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawazi kukubaliana na hali ya tz kwa sasa na wakiichua igunga ntashindwa kuwashangaa wana igunga na watz kwa ujumla
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Hatuna serikali kwasasa.
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Sep 29, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Serikali ya mpito ya ndugu kikwete Inatisha! Nimeshangaa kwanini wanatumia nguvu kubwa hivyo ilihali wao ndio wako madarakani yaani wangekuwa kuna la maana walilowahi kulifanya ungekuta ss wanakubalika automatically. wamevurunda maisha yamekuwa magumu kupitiliza, mahitaji muhimu hakuna, matokeo yake yote yamepeleka masaburi igunga, bila kujua they are loosing our money and time.

  Ule muda wa kuwajibika kwa ajili ya majukumu ya kujenga taifa Wassira anautumia kueneza propaganda za CCM igunga, na lingine liko huko New Delhi toka January na mshahara unaingia benki huku dar es salaam kodi za wananchi maskini zinazotumika kutibu mtu mmoja huko zingeweza kujenga hospitali ambayo ingetibu mamia ya watanzania...hawa . ccm...hawa.... lazima kuna siku tu moto utawaka!
   
 7. a

  abduel paul Senior Member

  #7
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Embu tujaribu kufikiri, mfano...! Uchaguzi umeshapita mbunge kachaguliwa awe toka UDP, CUF, CCM au CDM, then what? Igunga ni sehemu ya ngapi ya Tz yote? Hata tukasahau yanayoikabili nchi kwa ujumla?

  Vuguvugu la katiba mpya limefifia na pengine labda wapo wananchi ambao wamebadili hata mawazo na kuona haina haja tena, pengine hata baadhi ya wanaharakati,hayo ni machache ya matatizo ya kitaifa ambayo Tanzania yetu inayapa mgongo kila matatizo mapya yanapo ibuka, mfano hivi yupo anayeshangaa na kuugua juu ya kuzama kwa meli znz tena? Hata kukatufanya tujifunze na kutafuta tatizo km ilivyo kwa Mv bukoba??
   
 8. a

  abduel paul Senior Member

  #8
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo hii hata vyombo vya habari muelekeo wake ni mmoja tu, kama mi ningekuwa muwekezaji wa madini! Muda kama huu ningeamisha hata mkoa mzima wenye madini kupeleka ninapoishi, kwakua hakuna mwenye habari tena na mimi,
   
 9. a

  abduel paul Senior Member

  #9
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umeme unakuwepo mpaka pawepo na uchaguzi?? Hivi hakuna wataalamu wa kufanya tathmini ya shughuli za kisiasa kufanya tathmini ya faida na hasara ya siasa Tz ukilinganisha na nchi nyingine?
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  wataalamu wenyewe wanaendeshwa kama remote control akina Badra Masoud kimyaa wanatimiza malengo ya wanasihasa.
   
 11. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #11
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Muda wote mchana umeme haukuwepo mtaani kwetu, umeme umerudishwa kama saa 12 jioni, lakini kutoka saa 12 mpaka saa 2 usiku umeme umekatwa na kurudishwa zaidi ya mara kumi, tumelazimika kuzima kwanza vifaa vya umeme kwakuwa vikiunguwa Tanesco hawatalipa, lakini mbaya zaidi ni kuwa mgawo umeongezeka mara dufu, zamani siku za jpili ilikuwa si rahisi mtaani kwetu tukose umeme, siku hizi wanakata mpaka jpili. Ni vigumu kuzungumzia tatizo la umeme nchini, mi nafikiri vyombo vyote vya habari vingeandika habari moja tu ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho kuhusu umeme tu.

  Inasikitisha na kustaajabisha kuwa mali zote hizi ilizojaaliwa Tanzania bado nchi haina hata umeme!. Nimefikiria kuwa pengine wazungu wanapotuzomea kuwa sisi ni nyani huwa hawakosei kwa kuwa maisha tunayoishi ni nyani tu ndo walipaswa kuishi hivi na si binadamu. Madini ya kila aina na ya thamani, maji ya mito, maziwa, mabwawa, bahari, milima, ardhi nzuri, misitu, mbuga za wanyama, bandari; lakini bado Tanzania haina umeme!

  Wakati ule bajeti ya wizara ya nishati na madini ilipokataliwa na kutakiwa kuandaliwa upya umeme haukukatwa hata mara kama wiki 2 hivi, niliwaambia majirani kuwa subirini bajeti ipite mgawo zaidi ya uliopita, na ndicho kilichotokea!!

  Aibu TANZANIA HAINA UMEME. Mi nipo tayari UFISADI uendelee lakini watuachie UMEME kwakuwa kunapokuwa na umeme wauza juisi na vinyoozi wa saluni tunapata hela ya kununua dagaa, tunapoendelea kukosa dagaa sababu ya umeme mwisho itabidi tufe.
   
 12. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ni mwaka wa 6 kwa sasa inawezekana ikafifkia 10 katika hali hiyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  AP.... Kwa hali ya siasa ilivyo katika nchi za kiafrika kwanzia kwa majirani zetu (zambia na malawi) na ndugu zetu wengine huko uarabuni imepelekea uchaguzi huu wa Igunga kuangaliwa kama kipimo kikuu katika kuamua hatima ya vyama husika na siasa za nchi kwa ujumla.... Haya ndio mazingira ya ukweli, ni itakuwa kujidanganya kujaribu kutaka ku-overlook hichi kitu. Pia ni kweli siasa za nchi zote zinaendeshwa na matukio japo tuna mapungufu katika mgawanyo wetu wa kimfumo wa kusimamia matukio husika pasipo kuathiri sana program za nchi na ajenda maridhawa.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  hhahahahahaa wewe bana!!!
  [​IMG]
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  hivi yule binti ana akili nzuri kweli au ndio mambo ya kobe............ukiona kobe juu ya mti ujue amepandishwa huyo....kobe hawezi kupanda mtu bana!!
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu umeambiwa Igunga hakuna mgawo wa umeme! Serikali imehamia Igunga kwa muda.
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Just imagine ikitokea say uchaguzi kula baada ya miezi sita mpaka 2015!!!!!
   
 18. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Jumlishia na tozo tunayotakiwa kuilipa Dowans
   
 19. B

  Bukijo Senior Member

  #19
  Sep 30, 2011
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  NDIYO!
  Kwa sababu kila mtu naona yupo interested na siasa.
  Siasa nahisi inalipa kuliko secta yoyote inchini tz.
  Hayo nimejibu kulingana na hali halisi nianavyo mimi japo si mwanasiasa.Tazama vingozi wote wa nchi,vyombo vya habari n.k wapo Igunga.Wabunge vyama vyote wapo Igunga sijui kuna Bunge linaendela pale!
  Mimi nadhani kwa sasa wanasiasa walikuwepo wapo loose yaan hawana cha kufanya zaidi sasa wamepata kisingizio mahala pa kupiga porojo zao hasa baada ya Bunge kuisha.

  Wanasiasa ni sawa na Wachezaji wa michezo mbalimbali wakikaa bila Porojo zao hujisikia vibaya,hulemaa ndimi nzao na akili zao so mda wote wanapenda wawepo viwanjan kwan ndo furaha yao.
  Kwan Igunga inaliingiza pato la taifa asilimia ngapi had ipiganiwe vile?.Vyama vyote vinatumia nguvu kubwa,mala Helkpita zinatumika kule kwan Igunga ina KM square ngapi had helkpita zitumike?.
  Tanzaniaaa! Tanzaniaaaaaa!!!!!!!!!!!!! nakupenda kwa moyo wooteeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!! nchi yangu ....................................
   
 20. jameeyla

  jameeyla Senior Member

  #20
  Sep 30, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la siasa tanzania linaingilia mpaka utendaji wa kazi na uhuru wa mahakama,,leo malipo ya kuwalipa dowans ni kiherehere cha wanasiasa kuingilia utendaji wa serikali,kuilipa dowans tutawalipa kwa kuwa watu waliingia mikataba na wakasaini kwa hivyo kuvunja mkatabba ni hasara yao walipe dowans na mitambo iwashwe haraka ili kumaliza haya matatizo .igunga its another case.....
   
Loading...