Tanzania itajengwa na wahalifu tu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,309
12,604
Wazee nimewaza sana juu ya namna mambo yetu Tanzania yanavyotofautiana sana na mambo ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea kwa kasi. Bahati nzuri nimeshawahi kuishi kwa muda kwenye baadhi ya nchi hizo. Nimegundua kuwa Tanzania hatuna nyenzo za kuwawezesha wananchi kufanya maendeleo yao binafsi kwenye nchi yao kwa kufanya kazi halali bila kulazimika kufanya uhalifu wowote.

Mifano kwa nchi zinazoendelea na zilizoendelea:

1. Mishahara kima cha chini ni kati ya USD10 na 50 kwa saa moja la kufanyakazi, yaani TZS22,000 na 110,000 kwa saa moja.
2. Nauli ya daladala ni kati ya USD1.5 na 3 kati ya kituo hadi kituo, yaani TZS3,300 na 6,600
3. DVD ya muzic/filam ni kati ya USD10 na 20 kwa moja, yaani TZS22,000 na 44,000 kwa CD/DVD
4. Kikombe cha kahawa ni kati ya USD3 na 5, yaani TSH 6,600 na 11,000 kwa kikombe.
5. Parachichi moja ni USD3, yaani TSH 6,600 kwa moja.
6. Kunyoa nywele ni USD 20 na 30, yaani TZS 44,000 na 66,000 kwa kichwa kimoja kukinyoa
7. Hot dog ni USD 5 kwa moja yaani TSH 11,000
8. Soda ni USD 1, yaani TZS 2,200 kwa kopo
9. Mwanasoka analipwa kati ya USD 50,000 na 100,000 kwa wiki moja.
shoe shine ni kati ya USD 5 na 10, yaani TSH 11,000 na 22,000
10. Kodi ya mapato/VAT ni kati ya 4% na 8% inategemea na uko nchi/jimbo gani.

Hebu linganisha viwango hivyo hapo juu na hivi vya kwetu hapa nchini halafu uone ni kwanini wenzetu:
1. Wanapenda kufanya kazi za aina yoyote bila kuchagua wala shuruti
2. Hawakwepi kodi
3. Wanatajirika hata wakifanyakazi ya aina yoyote ile hata iwe ya kinyozi, kuuza bagia, sanaa, daladala, kilimo.
4. Wanazipenda nchi zao

Hii ina maana kuwa mishahara yetu, kodi zetu na bei za vitu na huduma zetu havina uhalisia wowote, hivyo kusababisha uwezekano wa Tanzania kupenda
1. Kuchagua kazi
2. Kukwepa kodi
3. Magari ya abiria kuvunja sheria za barabarani ovyo, yaani nauli ya daladala ni sh. 400, yaani USD 0.2 na Dar hadi Arusha USD13.6 tu. Biashara ya aina hii haiwezekani kabisa kumtajirisha mtu
4. Watu hawataki kwenda kulima maana bei ya mazao yao ni ndogo mno kuliko gharama halisi za uzalishaji
5. Kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu kama rushwa, wizi, na ufisadi ili kutafuta uhalisia wa maisha.
6. Kujenga kiholela kwenye viwanja visivyopimwa na makandarasi wa ujenzi hafifu/wakienyeji
7. Kununua vitu used/mitumba au bidhaa feki za "kichina"

Piga hesabu kwa wale umilokuwepo zamani, mishahara ya wakati ya Rais Nyerere ilikuwa mikubwa sana kuliko mishahara ya sasa kama ingekuwa inalipwa kwa dollar za Kimarekani au pound tangu awamu ya kwanza.

Nadhani iko haja ya kuyapanga upya maendeleo yetu vinginevyo tutalaumiana bure hapa kwa kudhani kuwa huenda mtawala fulani akiingia madarakani basi mambo yetu yooote yatanyooka, shida hapa siyo mtawala bali mfumo umeharibiwa kabisa huko nyuma wakati idadi yetu ilipokuwa watu 9mil tu, sasa tuko 50,000,000. Sasa hivi watu wote wanaofanyakazi, biashara na kilimo halali wamepoteza uwezo wao wa kununua, kutoa na kugharimia huduma unzuri. Ni walifu tu ndiyo wenye uwezo wa kujenga jumba refu
 
Sasa Moshi to Arusha more than 75 km haifiki Tsh 5000 cha kushangaa hapo ni kipi?
Ilipaswa iwe zaidi ya sh. 5000 ili mwenye basi amudu gharama za uendeshaji wa gari lake kama mishahara ya dereva, kondakta, uniform zao, service, kodi na matengenezo ya gari, chakushangaza hapo ni kwanini bei iwe chini ya sh 5000 halafu unategemea basi kama hilo liwe level seats.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom