Tanzania ipi tunaitaka?

Tanzania ipi tunaitaka?

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,970
Nawasalimia wana JF.
Nimekuwa nikijiuliza sana kwa kina hivi nchi yetu tunataka iwe kama nchi ipi?
Je kama Kenya, USA, China, Uingereza, Afrika ya kusini, Naijeria au kama nchi ipi?
Maana watu wengi wamekuwa wakilinganisha nchi yetu wakisema angalia wenzetu wamefanya hili na lile.

Hapa nataka niongee kitu hiki, Je nchi yetu tunataka iwe kama nchi ipi?
Ukisema tunataka kufanana na China, hapa hapatakalika maana unajuatena China wako na chama kimoja na sheria zao kari je tutaweza hayo?

Ukisema tuwe kama Kenya hapa ndio watu hatutaelewana kabisa maana hao wenzetu wana ukabila kama nini.

Sasa tuwe kama Uingereza, Dah hapa mila zetu hazitaturuhusu maana yake tukubali ushoga

Basi tuwe kama Nigeria: hapa ndio kabisaaa maana ugomvi wa kidini kila kukicha watu kuuana kama wanyama.

Sasa tuwe kama Marekani uwi hapa ndio pagumu maana uadui wao ni wa kudumu na waarabu, wakorea kwa hiyo mda wowote tutegemee maajabu.


Sasa nchi yetu iweje? Maana kila ukionacho kizuri kwa wenzako utadhani ni kirahisi huwa kina gharama yake.

Nadhani tuhusishe jamii zetu na tamaduni zake ili tuunde nchi yenye utamaduni wake.
 
Back
Top Bottom