Tanzania International University,,,unakijua hiki CHUO???

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Wadau leo nimekatiza maeneo ya Kimara,safar yangu ikiwa kuelekea KIMARA BONYOKWA,ila kuna ya kuingilia barabara ya kwenda bonyokwa upande wa kushoto nimeona jengo la ghorofa 3 au 4,ni leupe limeandikwa kwa maandish makubwa ya rangi ya blue'TANZANIA INTERNATIONAL UNIVERSITY,then kuna admission block,kwa bahat mbaya sikumuona mtu wa kumuuliza,
ila nataka kujua wenzangu kwenye list ya TCU hiki chuo kipo????
 
kama haja ni hiyo tu, visit web ya tcu utaona list. ila vyuo ni vingi kama utitiri, sijui waheshimiwa hawalioni hili? halafu vina maina mazuri balaa, ipo siku utasikia harvard university tanzania
 
mh..hi ndo tz bwana...hata mimi mwakani ntaanzisha chakwangu.
 
nilikuwa najaribu kupitia list ya vyuo vilivyoorodheshwa na TCU baada ya kusoma status yako...hiko chuo hakipo....labda ndo wanataka kukiestablish...heheee....though ni vizuri kama bongo itakua na vyuo vingi vya kutosha, ila viwe vmesajiliwa na kutoa elimu nzuri..
 
HIVI huwa hakuna restrictions ya matumizi binafsi ya majina kama TANZANIA, TANGANYIKA, ZANZIBAR, KILIMANJARO n.k n.k ?
Amini usiamni unaweza kukuta hicho chuo ni cha kufunza vitu vya ajabu ajabu visivyo na tija kwa Taifa na wala havibebi hadhi sawa kama jina lilivyo...
 
Yap.hiko chuo kipo ila hakijaanza kupiga mzigo na kwenye list ya tcu hakimo.zina elezeka habari kuwa kilikoa ela kikakwama,kwamba ndo kimepata wafadhiri kianze kazi.wanategemea kuamza na ngazi ya cheti ktk fani mbalimbali then diploma then digrii mwaka huu mwishoni.la kushangaza kinatoa huduma ya kozi kama mia mbili kuanzia cheti.fatilia mpunga huo
 
Ni vyema tukawa na vyuo vingi ili kuondokana na urasimu uliokuwepo awali, lakini pia uwepo huu waendana na ongezeko la wahitimu katika kidato cha sita. I see no problem if all is done under the armbit of the laws of this country.
 
Wadau leo nimekatiza maeneo ya Kimara,safar yangu ikiwa kuelekea KIMARA BONYOKWA,ila kuna ya kuingilia barabara ya kwenda bonyokwa upande wa kushoto nimeona jengo la ghorofa 3 au 4,ni leupe limeandikwa kwa maandish makubwa ya rangi ya blue'TANZANIA INTERNATIONAL UNIVERSITY,then kuna admission block,kwa bahat mbaya sikumuona mtu wa kumuuliza,
ila nataka kujua wenzangu kwenye list ya TCU hiki chuo kipo????

http://www.tcu.go.tz/images/pdf/TanzaniaInternationalUniversity.pdf
 
"HUO NDO UHURIA WA SOKO HURIA"! Hebu fikilia walipataje ujasiri wa kujitangaza kabla hata hawajasajiliwa? Au kwa nini walichagua jina kubwa kiasi hicho eti Tanzania International University! tusishangae sana kwani kuna hata makampuni ya kutengeneza pombe yalisha tangazia Duninia eti urithi wetu(Watanzania) ni pombe!
 
Jamani nina taarifa za uhakika kuwa TCU wamekipiga stop Tena leo.angalieni kwenye Itv facebook.utakutana na hiyo habari wameiweka . jamaa walikuwa wameshaendesha zoezi la kuajiri walimu
 
Karibu mjini!
Chuo kina mda mbona.
Ma graduates tupo tuna kazi kitaa
 
:yo:Kila siku vyuo vikuu vinaongezeka lakini swali la kujiuliza je ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo hivyo inaendana na hali ya soko la ajira?.Tusije tukawa tunamrundikano wa vyuo vikuu lakini tukawa na idadi ndogo ya watu walioelimika na kuwa na uelewa sahihi kulingana na taaluma zao, ndio hao wanaoteketeza taifa kwa utendaji mbovu makazini kutokana na kuzalisha degree holders wasiokua na sifa linganishi na taaluma zao.issue iliyopo ni kujipanga na sio kukurupuka kufungua vyuo kwa masilahi ya watu binafsi na kuzalisha wasomi feki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom