Tanzania inaweza kuongeza bei ya kahawa kwa kuwatumia kinyesi cha " Civets"-Fungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania inaweza kuongeza bei ya kahawa kwa kuwatumia kinyesi cha " Civets"-Fungo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Hofstede, Aug 12, 2009.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kahawa inayotengenezwa kutokana na kinyesi cha Fungo "Civet" ni kahawa ambayo ni most expensive in the world. Kikombe kimoja hugharimu mpaka USD 65. Nchi za Indonesia zimekuwa zikiwatumia wanyama hawa ambao wamejaa sana Tanzania katika kuipa ubora kahawa yao.

  1. Fungo-"Civet" ni mnyama gani?.
  Kwa wale waliowahi kuishi au ambao wanaishi vijiji mbali mbali Tanzania watakuwa wameshakutana au kusikia neno fungo. huyu mnyama inasemekana ana sifa kuu moja, yeye huchagua sehemu maalum ya kujisaidia, yaani hata kama akiwa umbali wa mile kumi akijisikia haja hukimbia mpaka eneo lake. Watu wengi wameisha wahi kukuta lundo la kinyesi cha hawa wanyama sehemu moja ama nyingine porini ."mavi ya fungo"- huwa na mbegu za matunda aliyomeza ambazo hazisagwi tumboni "partially digested faeces"

  2. Jinsi gani Fungo anaongeza ubora kwenye kahawa?
  Civets hupewa diet ya mbegu za kahawa na kuzimeza au kula kama chakula chao, ambazo huwa partially digested, pindi wajisaidiapo hutoka kahawa mbegu, ambazo huoshwa kukaushwa kukaangwa na kusagwa, kahawa hii ina taste ya kipekee na nzuri na ndiyo chanzo cha kuuzwa ghali. Nchini Indonesia kahawa hii hujulikana kama "Kopi Luwak"

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=1Q7IYpLYQ7Q[/ame]

  Kwa kweli tunaweza kuwatumia wanyama hawa kuongeza ubora kwenye kahawa yetu ambayo inashuka bei kwa kasi. Kinachotakiwa ni kuwekeza katika research na kuwafuga hawa wanyama kwa wingi badala ya kulalamika bidhaa zetu zinashuka bei kwenye soko la dunia.
   
 2. M

  Maquiseone Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa kweli sidhanii hata kama hii itaendelezwa hata kama ikiwa na maana, maana sio utamaduni wa watu wetu kushulikia reseach. Watakula pesa za walala hoi then jii. jiulize mradi wa kuyaangamiza magugu maji kwa wadudu umefikia wapi? Na wadudu wapo wengi mno na watu walirushwa nje kama wehu, fund zote kwisnei na mambo jii. Sasa huu labda wajaribu wadau wenyewe kwa kujiongezesa kipato kama wajasiriamali
   
Loading...