Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,610
Asitokee mtu akamdanganya mtanzania kwa namna yoyote ile, ushiriki wetu wa michuano ya mataifa huru Afrika ni muhimu kuliko siasa za kisasa za vyama vingi. Kuonekana kwetu katika michuano hii ya soka ambayo hukutanisha timu bora za mataifa ya afrika ni muhimu sasa pengine kuliko katika kipindi chochote nyuma.
Tulionekana mara ya mwisho tukishiriki AFCON mwaka 1980, miaka 39 iliyopita. Sio jana wala sio juzi, enzi hizo magari unayahesabu jijini Dar. Unatoka na basi la Yarabi Salama pale kisutu kituo cha mabasi cha zamani saa moja kasoro jioni unafika Tanga kituo cha mabasi saa moja kamili asubuhi inayofuata. Unatuma barua kwenda Kigoma au Rukwa inafuka baada ya wiki mbili.
Marais kuanzia wa awamu ya tatu mpaka hii ya tano wamejitahidi sana kuitangaza Tanzania kiuchumi lakini uchumi pekee pasipo nchi kuwa na uwezo wa kujitangaza yenyewe kupitia michezo ni jambo gumu kufanikiwa.
Kuna watu wanasema hawawezi kuiunga mkono Taifa Stars ikicheza dhidi ya Uganda Cranes eti kwa sababu waliopewa kazi ya kuamsha hamasa ni watu wenye dhambi kadhaa. Wanachosahau ni kuwa Tanzania ni kubwa na yenye thamani kuliko hawa wanajamii wa kisasa ambao mwaka 1980 wakati kina Tino na Ngulungu wanapambana kule Lagos walikuwa aidha ni wadogo sana au hawajazaliwa.
Tanzania inahitaji sana wimbo wake wa Taifa upigwe mbele ya hadhira nzima ya wapenda soka wa Afrika, litakuwa ni jambo ambalo litautangaza utalii, litainua upya kiburi cha kitaifa kwamba nasisi tunaweza kile kinachoweza kufanywa na muafrika mwingine yoyote. Kizazi cha sasa chenye wenye nguvu ya kuzalisha kitakuwa kimepata heshima mpya.
Hapo sijaongelea soko la wachezaji, la hawa wadogo zake Mbwana Samatta na Simon Msuva. Sijaongelea soko la makocha wazalendo. Sijaongelea changamoto watakazozipata Simba na Yanga katika kuendana na dunia ya kisasa isiyomsubiri mtu asimame na kujikung'uta, yenyewe ikienda mbio muda wote.
Yapo mengi mno na muhimu tutakayoyapata ikiwa tutafanikiwa kushiriki AFCON kule Misri.