Tanzania inaugua

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Bila ya shaka hakuna ubishi kuwa nchi yetu sasa inaugua maradhi makubwa, pengine ni maradhi makubwa zaidi ya ukimwi. Ufisadi, mfumuko wa bei za vyakula unakua kila siku wakati wenzetu wanaojiita ndio watawala wa nchi hii wanakula kuku kwa mrija. wiki hii nimepata bahati ya kufika katika kijiji kinachoitwa Kubi ambacho kipo mpakani mwa Kondoa na Singida kwa upande wa kusini magharibi mwa Kondoa, kwa ukwli hali ni mbaya sana huko. lakini kuna watu wanaishi, wanaishi kama wanayama wa porini.Serikali nayo ipo ikiwatazama kwa dharau kama tembo amtizamavyo sisimizi. tupeni macho yenu huko Libya, Tunisia na Misri, lakini hatutaki kufika huko. nchi yetu ya amani. je, mnataka kuivuruga?
 
Hizi biashara zingine- kazi kweli kweli. Any way labda tukuulize tu hilo jimbo Mbunge ni wa chama gani?
 
Umekuja kuuza kitabu au unahoja ya maisha ya watu huko Singida? Matatizo unayosema umeyaona huko kwa taarifa yako ndiyo matatizo ya watanzania wengi huko vijijini bila kujali ni eneo gani
 

Kwa uandishi wa hivi,walahi kitabu chako hata bure sichukui.
 
Tumeuzwa kwa waarabu kwa suti pea tano tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…