Tanzania inatarajia kuanza kutumia kinga ya HIV

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
993
Reaction score
1,882
‎Katika kipindi ambacho mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI yamekuwa yakitegemea nidhamu ya matumizi ya kila siku ya dawa za (PrEP), au wengi wanavyo ziita kama ARV,

‎Sasa Tanzania inaanza kuingia katika hatua mpya ya kinga ya muda mrefu kwa kuanza matumizi ya Lenacapavir, dawa inayodungwa mara moja kila baada ya miezi sita kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya HIV.

‎Hatua hii inawasilisha namna mpya ya kinga inavyotolewa na kupokelewa katika jamii.

‎Lenacapavir, iliyotengenezwa na kampuni ya dawa ya Marekani Gilead Sciences, ni dawa ya kundi la “capsid inhibitors” inayofanya kazi kwa kuzuia hatua muhimu katika mzunguko wa uzalishaji wa virusi vya VVU. Tofauti na PrEP ya kila siku kama Truvada au Descovy, sindano hii hutolewa mara mbili tu kwa mwaka.

‎Katika majaribio ya kimataifa, ikiwemo tafiti zilizohusisha wanawake na vijana barani Afrika, dawa hii ilionyesha ufanisi mkubwa sana katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU, hali iliyoibua matumaini mapya katika mikakati ya afya ya umma.

‎Utekelezaji wake nchini Tanzania umeanza katika mazingira ya tahadhari na tathmini ya karibu, ukilenga makundi yaliyo katika hatari kubwa ya maambukizi. kwa miaka mingi, changamoto kubwa katika kinga ya VVU haikuwa tu upatikanaji wa dawa, bali mwendelezo wa matumizi. Watu wengi walishindwa kudumisha matumizi ya kila siku kwa sababu za kijamii, kiuchumi, au unyanyapaa.

‎Sindano ya maramoja kwa miezi sita inabadilisha hali hiyo: inahamisha mzigo wa nidhamu ya kutumia dawa kilasiku kwenda katika ratiba ya kliniki iliyopangwa mara mbili tu kwa mwaka.

‎Katika muktadha wa Tanzania ambapo juhudi za kupunguza maambukizi mapya zimekuwa zikiendelea chini ya mipango ya kitaifa kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa, kuanza kwa matumizi ya Lenacapavir si tukio la kifamasia pekee bali ni jaribio la kuona kama muundo wa utoaji wa huduma unaweza kuathiri tabia ya kinga.

‎Kwa kuanzishwa kwa dawa hii, Tanzania inaingia katika awamu ambayo kinga ya HIV inaweza kupatikana kwa kwenda hospitali mara mbili tu kwa mwaka. badala utaratibu uliozoeleka wa kutumia dawa kila siku.


‎Ikiwa utekelezaji utaonyesha mafanikio katika kupunguza maambukizi mapya, hatua hii inaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa mkakati wa kitaifa wa kuzuia HIV na kuonyesha kwamba katika mapambano dhidi ya janga la muda mrefu, ubunifu wa ratiba tu unaweza kuwa na umuhimu kuliko ilivyokuwa ikidhaniwa.
 
Wasije wageuza watu mazombie tu.

Si karibu dunia nzima watahitaji hiyo chanjo.
 
Hivi bado kuna watu mnaamini hii SCAM(Drama) kuhusu ukimwi!?,peleka hizi story serikali ya China au ujerumani kama hujaonekana kituko.
 
Kama nawaona walugulu, na wanavopenda mizagamuo.. Muda wote lazima iwe ndani
 
Alternative nyingine ni kutochukua hiyo dose na kuendelea kupiga kavu, chaguo ni lako
AIDS = ARV'S, ukiambiwa una ukimwi usimeze ARV'S, kale vizuri wiki 3, nenda kapime kokote ulete majibu.
NB:, Usipopima ukimwi hutakaa uwe na ukimwi, .
 
AIDS = ARV'S, ukiambiwa una ukimwi usimeze ARV'S, kale vizuri wiki 3, nenda kapime kokote ulete majibu.
NB:, Usipopima ukimwi hutakaa uwe na ukimwi, .
Fafanua inamaana hakunaga gonjwa la ukimwi
 
Kwamba mwenye HIV akitumia hiyo sindano haambukizi wengine kwa vyovyote vile?
 
Fafanua inamaana hakunaga gonjwa la ukimwi
Mkuu UKIMWI ni upungufu wa kinga mwilini, upo miaka yote tangu Dunia iumbwe na utakuwepo miaka yote, kupungukiwa kinga ni kawaida kwa mwili baada ya muda mwili una recover, kuna ugonjwa ulijitokeza miaka ya 80 ukapatiwa dawa, ila wamarekani wakatembelea nyota mpaka leo kama ilivyotokea kwa COVID, wakaleta ARVs ukianza kuzitumia zinakuondolea kinga asili unaanza kuzitegemea ndo maana baada ya miezi mitatu ya kutumia ARVs ni ngumu kuziacha. Ukiambiwa una ukimwi kale vizuri baada ya mwezi kapime hospitali yoyote kama utakuta kitu. Story ni ndefu, tafuta documentary inaitwa HOUSE OF NUMBERS ipo YouTube, itakupa mwanga kidogo. H.I.V doesn't exist, it's a SCAM.
 
Ok ngoja niitafute hii documentary
 
Muda si mrefu, watu negative watabaki negative.
Moja ya malengo yao ni kufika 2030 if am not mistaken hakutakuwa na maambukizi mapya so wa huku wa huku wakule wa kule..unao unao huna huna kiranga chako tu ndio kitakuponza kuapata maambukizi mama endapo kinga/chanjo haitatumika
 
Naogopa hizo chanjo..sjui kinga zisijetafuta kinga ya mwili na kunipa janga jipya ndani ya mwili wangu woooi
 
Wewe ni SCAM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…