Tanzania inapambana na biashara ya kuuza "UNGA"????

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,743
Points
0

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,743 0
Kwa muda mrefu sana watanzania tumekuwa tukisikia watu mbalimbali wakikamatwa kwa makosa ya kukutwa na kete au mafurushi ya madawa ya kulevya,,,,,,mfano mmoja wapo ni jana ambapo kikosi cha madawa ya kulevya kimekamata zaidi ya kilo 90 za heroin zenye thamani ya bilion tatu.

Mara nyingi hawa watu wanapokamatwa huwa tunatangaziwa na kuoneshwa ule mzigo,,,,,lakini sasa kinachofuata baada ya hapo huwa mara nyingi hakisikiki. Hukumu juu ya watu hawa huwa watanzania hatuzisikii, ndio maana nikauliza je ni kweli tunapambana na biashara hii haramu?

Kwenye harakati za kuteketeza bangi huwa tunaoneshwa lakini sijawahi kusikia "unga" ukiteketezwa na waandish wakaitwa,,,,,,,,,Jana serikali ya Iran imetangza waziwazi kuwa imewanyonga watu zaidi ya wawili ambao walikutwa na hatia ya kuingiza "unga" nchini humo,,,,,,

Naskia hata china wakikutwa na hatia huwa wananyongwa,,,,,je Tanzania hapa adhabu inayotolewa kwa wauza unga inastahili?
 

Forum statistics

Threads 1,382,433
Members 526,380
Posts 33,828,486
Top