Tanzania inahitaji tafiti nyingi za wanataaluma wake ili kubaini hali yake ilivyo kiuhalisia

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,578
3,484
Nimestushwa sana na Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia na kuonesha hali ya umasikini kupungua Nchini kwa vigezo kama umiliki wa simu na mali nyingine.... najiuliza hivi kweli vigezo hivyo ndiyo vinazuia picha halisi ya maendeleo yetu?

Kuna haja ya wanataaluma wa Nchi hiii kuwajibika na kuacha kuendelea kuharibu. Hivi inaaingia akilini kwamba ukimiliki simu ndiyo maendeleo tunayoyataka Watanzania? ni utafiti upi ulifanyika ukaonesha Watanzania wakimiliki simu ndiyo watakuwa wamepunguza umasikini? Vigezo kama hivi vinatumika kwa sababu wanataaluma wamelalala wanasubiri kulalalamika.

Hii Nchi ili iendelee haihitaji sauti ya mtu mmoja tu katika kukemea na kukataa maovu kama anavyofanya Mheshimiwa Rais Dr.John Joseph Pombe Magufuli ila inahitaji kila mwanataaluma kuwajibika kikamilifu katika nafasi yoyote ile aliyopo.

Ni mambo yanayoshangaza sana na kutia huruma yanafanyika katika Taifa letu huku wanataaluma wakiangalia na wengine kuchangia katika kufanya mambo hayo ambayo kwa kweli yanasikitisha.
Rais wetu anapaswa kushauriwa vizuri na kwa ushawishi wa kutosha juu ya anachokifanya kwa sababu Taifa letu hatuwezi kuendelea kwa kutekeleza mipango ya mabeberu.

Jana nilisikitika sana kwenye mdahalo wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru ambapo niligundua kuwa hata Muono wa Taifa letu "Vision 2025"ulifadhililiwa na mabeberu na huenda tunatekeleza wanayoyataka wao hata sasa na siyo hasa matakwa ya Watanzania.

Kujua Watanzania wanataka nini hasa siyo jukumu la mtu mmoja tu mfano Rais na Serikali yake la hasha!.ila ni jukumu la wanataaluma kufanya tafiti za kutosha katika kila eneo na kupata mchango wa kila raia katika kila eneo.
Mathalani kuhusu "Uchumi wa kati na wiwanda"tujiulize Watanzania wanataka nini hasa kwenye hivyo vitu na je kama ni viwanda kunahitaji viwanda vipi hasa?

Tuna faida zipo za kiushindani "competitive advantage "ambazo tumefanya tafiti na kuziona kuwa zinatusadia kukuza soko la bidhaa za viwanda vyetu?

Sawa tunatakaka Tanzania iwe ya viwanda lakini tujiulize tunahitaji viwanda vya aina ipi katika wakati huu.Je tunataka viwanda ili miradi viwanda kwa kuhesabu idadi tu au tunahitaji viwanda kulingana na mahitaji ya Watanzania na pia soko la ushindani?

Mataifa makubwa yote yaliyoendelea kiviwanda yalitengeneza sera na mkakati madhubuti ya kulinda viwanda vyao kwa makusudi kabisa na sisi tujiulize tuneandaa mazingira ya kulinda viwanda vyetu kwa kiasi gani?Maswali kama haya na mengineyo ndiyo maswali ambayo wanataaluma wa Taifa hili wanapaswa tujiulize na kuyafanyia tafiti ili kuonesha sauti halisi na hali halisi ya Taifa.

Katika kulizungumzia Taifa haihitaji mwanataaluma kutumia itikadi yake au chama chake ila inahitaji kutifungamana na upande wowote ule isipokuwa uhalisia unavyotaka .

Wanajamii wamekosa imani kabisa na aina ya Wanataaluma wa leo kutokana na mambo yanavyoenda na juu ya hili haihitaji tafiti kujua kuwa jamii imeanza kuwadharau wanataaluma ila jaribu kuangalia tu hata Rais anapowawajibisha wanataaluma ambao ni viongozi katika maeneo mbalimbali kwa kuwaonya au kuwakaripia cheki jamii inavyoitikia utagundua tu.

Kwa kiasi kikubwa Taifa letu limefikishwa hapa na Wanataaluma.Hali tunayoiona ni zao la muenendomzima wa matendo ya Wanataaluma.

Inasikitisha sana.
 
Moja ya kiashiria cha maendeleo ni kuongezeka kwa kwa mawasiliano kirahisi kwa iyo kwa utafiti huo unaweza kuwa wako sahihi kusema ivyo ingawa vipo na viashiria vingine vingi kama kuongezeka kwa umri wa kuishi,kupungua vifo vya watoto na wamama wajawazito, kipato cha mtu kwa Siku,upatikanaji wa huduma za afya kiukaribu,
Kwa nchi yetu tunapo elekea ni pazuri kikubwa tufanye kazi porojo nyingi hazitatufikisha popote
Kwangu mimi Rais wetu wa sasa anatupeleka mahali salama tuvumiliane
 
Moja ya kiashiria cha maendeleo ni kuongezeka kwa kwa mawasiliano kirahisi kwa iyo kwa utafiti huo unaweza kuwa wako sahihi kusema ivyo ingawa vipo na viashiria vingine vingi kama kuongezeka kwa umri wa kuishi,kupungua vifo vya watoto na wamama wajawazito, kipato cha mtu kwa Siku,upatikanaji wa huduma za afya kiukaribu,
Kwa nchi yetu tunapo elekea ni pazuri kikubwa tufanye kazi porojo nyingi hazitatufikisha popote
Kwangu mimi Rais wetu wa sasa anatupeleka mahali salama tuvumiliane
Kama umelipitia vyema andiko hili kuna mahali nimeandika Rais anahitaji ushirikiano na wanataaluma na siyo kuupambana peke yake.
Wasomi wanatoa mchango upi kwenye jitihada za Rais nadhani ndiyo suala hasa la kijiuliza na juu ya tafiti zilizotolewa na vigezo vyake view sawa au si sawa bado tunapaswa kujua tafiti za wanataaluma wetu zinasemaje?.
 
Back
Top Bottom