Tanzania inahitaji Bunge Linaloning'inia (Hung Parliament) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania inahitaji Bunge Linaloning'inia (Hung Parliament)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, May 7, 2010.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huku hali ni tete baada ya uchaguzi wa aina yake kuleta matokeo ambayo hayajawahi kutokea kwa muda mrefu - kuwepo wa bunge linaloning'inia. Nadhani nasi tunahitaji bunge la aina hii huko nyumbani katika kipindi cha mpito kuelekea 2015. Hivyo ndivyo linavyokuwa:

  What is a hung Parliament?
  When no single party wins an overall majority after a general election — that is 326 or more MPs out of 650.

  Endelea kusoma hapa: http://www.timesonline.co.uk/tol/news/politics/article7119706.ece
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  INAWEZEKANA , lakini lazima elimu kwa Umma iendelee kutolewa kuwa CCM sio chama cha Serikali, chama chochote kinaweza kuunda serikali, Lazima watu wetu waamke, waamini kuwa bila CCM nnchi inaweza kwenda mbele.
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bendera ya CCM ibadilishwe; wafanyakazi wameshakataliwa na CCM; wasomi walishatupwa kule (wanafunzi wa vyuo na cost sharing),Ibadilishwe sasa WAFANYAKAZI sio sehemu ya CCM tena; Hii ndio ajenda mhimu sana jamani 2010; bendera ibadilishwe; napiga yowe sasa benderfa ibadilishwe; au tuwarushie mchanga wenye bendera hiyo tukiwaona maana imekosewa
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0

  Mkuu usijidanganye kwa Tanzania hilo ni ndoto mpaka yafuatayo yatokee.
  1. Tume huru ya uchaguzi itakayokuwa na kauli ya haki,haki tupu bila ya kuingiliwa na watawala. Tanzania iliharibiwa na Nyerere 1995 alipofunga safari ya siri kwenda kumuona mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar na kumtaka atangaze Salmin Amour kashinda badala ya yeye mwenyewe ku-admit kuwa ameshindwa, hiyo ilikuwa ni demonstration tosha ya mwanzo kwa kutumia uchanja na nafasi za walio na madaraka kubadili matokeo ya uchaguzi na kutumia nguvu za vyombo vya dola kunyamazisha wananchi. Hakuna uchaguzi hata mmoja uliowahi kutoa matokeo halisi ya matakwa ya wananchi Tanzania tokea tuanze demokrasia ya vyama vingi.

  2. Demokrasia inapiganiwa haiombwi, ni pale watanzania watakaposema enough is enough na kulazimisha watawala kufuata matakwa yao, hili haliwezi kutokea kwa kupiga kura kwa vyama mbadala bali kuionesha CCM kuwa bila haki na kusikia matakwa ya wananchi none us will be happy in this country hata awe na mamilioni ya fedha.

  3. Mwisho ni elimu kwa wananchi na utashi wa dhati kwa viongozi wabinafsi ambao wanaona wakitolewa madarakani basi kurudi ni ndoto, maana kama wao walikuwa wanatumia dola kushinda na wapinzani wakishinda watakuwa hivyohivyo, kwa maana hiyo USHINDI NI LAZIMA, wapiga kura watuchague wasituchague.


  TUJENGE UTAMADUNI WA KUHESHIMU MATAKWA YA WAPIGA KURA SIYO MASILAHI YA CHAMA KINACHOONGOZA LEO. TUKIFANYA HIVYO NINAJUA KUWA CCM NA VYAMA VYOTE HAVITAKUWA NA WSIWASI KWANI WANAJUA KUWA NIKINYIMWA KURA UCHAGUZI HUU ALIYECHAGULIWA ATAPEWA KURA TENA KWA KUTEKELEZA ALIYOYAAHIDI, VINGINEVYO WATANIRUDISHA MIMI. TUKIFIKA HAPO NCHI YETU NDANI YA MIAKA KUMI ITAKUWA IMEENDELEA NA KILA APEWAYE DHAMANA YA UONGOZI ATAJARIBU KUITUMIA VIZURI KUONESHA KUWA YUPO KWA MASILAHI YA WAPIGA KURA

  My take: Naipenda sana nchi yangu na ninapenda amani tuliyonayo kwani ni msingi wa ustawi na maendeleo yetu, ila kama kuna kundi linatumia mwanya huo kuhujumu nchi kwa kuwa tu sisi ni waoge, basi itakuwa ni hatua kubwa sana kama wakiwa wakipanga kete zao wanajua wazi kuwa watanzania si waoga tena tuwatendee haki ili Imani yetu idumu, basi hapo patakuwa na uwezekano wa kuwa na "HUNG PARLIAMENT"
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  1. Ndo umeshtuka leo?
  2. Na kukitokea hivyo...nani ataunda serikali?
  - Kumbuka sisi tuna Rais (ambaye anaweza kutoka Chama A) na bunge (linaloweza kuwa na majority ya Chama B)
  Kwa hiyo nani ataunda serikali - Rais au Bunge
  Je Katiba inatoa mwanya wa Vyama vyetu ku-negotiate, na kutengeneza serikali ya minority?
  Hii inazalisha swali la tatu;
  3. Je tunazijua kwa undani philosophies za vyama vyetu, kiasi cha kujua ni vyama vipi vinaendana kisiasi? Kwa mfano, Chadema na CUF wanaweza kuunda serikali pamoja?
  Swala la wagombea binafsi nalo lazima litazaliwa upya
  4. Je mbunge binafsi, ataweza kuingia katika serikali?
  5. Na serikali yenye wabunge binafsi itakuwa answerable kwa nani?
  - ni hayo machache kwa sasa tu

  Mwisho wa siku, WaTz hatujui Uraia, na jinsi nchi yetu inavyoongozwa! Labda imefikia wakati muafaka wa kurudi darasani na kujifunza upya!
   
Loading...