Tanzania inaelekezwa kaburini

ngozimbili

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
1,398
1,006
Mfululizo wa matukio unaonyesha kuwa nchi yetu imeianza safari rasmi ya maangamizi,vitisho,mauaji,uteswaji wa raia katika namna ambayo haijawahi kutokea kabla,milipuko ya mabomu kuanzia kwenye mikutano ya kisiasa mpaka kwenye nyumba za ibada.kumwagiwa tindikali mashaikh mpaka risasi mapadre,kutoka kwenye uandikishaji mbovu na wasiwasi wa kutofanyika uchaguzi mkuu,yote haya hayana majibu ya kisayansi kutoka kwa dola mpaka vyombo vya dola.nchi imekuwa ya vitisho tu,vitisho vya ugaidi,vitisho mwanasiasa fulani akipata urais,vitisho huyohuyo akikosa urais,vitisho waislam wabaya,vitisho mfumo kristo,vitisho,vitisho Taifa kaburini
 
ni wenye haki ndio wataliokoa lisiingie huko ila kwa uwezo wa Mungu tuu
 
nimemsikia Rpc wa Iringa anaongea kwa Vitisho na Shari nyingi wakat walikuwa wanatuliza wananchi ambao wanadai barabara iwekwe matuta baada ya mwanafunz kugongwa gari, najiuliza hawa Polisi wapo kulinda usalama wa raia au WANAPAMBANA NA RAIA??!
 
Back
Top Bottom