Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,607
- 46,245
Ukifuatilia kwa makini utagundua kuna ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi, majirani na wengine wengi wanaotuzunguka kwa maneno wanayosema, vitu wanavyoamini au baadhi ya vitendo wana matatizo ya akili na hivyo kuhitaji huduma za afya ya akili kupitia wanasaikolojia na madokta wa afya ya akili "psychiatrists". Hata wewe binafsi unaweza kujikuta katika hali ya matatizo ya aina hiyo.
Kila mara huwa nasikia Mirembe ikitajwa kila inapozungumzwa matatizo ya akili.
Ningetaka kujua kwa wanaofahamu kama kuna Hospitali nyingine zaidi ya Mirembe za serikali au binafsi zinazotoa huduma za afya ya akili.
Pia serikali ina sera au muongozo wowote unahohusu kushugulikia wagonjwa au wenye matatizo akili?