Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,811
- 107,299
Hakuna chochote cha msingi kilicho tofauti alichofanya Magufuli ambacho hakikufanywa na Sokoine.Magufuli alionyesha utofauti kama kiongozi tangu mwanzo wa safari yake ya uongozi na siasa.Katika ngazi zote za utendaji na kama Waziri,alitimiza wajibu wake katika kila eneo.Akawa kivutio kikubwa kwa wananchi na hata adui zake ndani na nje ya nchi.
Kwa siri adui zake walikiri umahiri wake katika utendaji,ingawa hadharani,walionyesha chuki dhidi yake.Magufuli hakuwa fisadi.Hata hivyo adui zake walijaribu kila walipoweza kumpaka matope,ili aonekane kwamba naye ni fisadi na ana tabia za hovyo kama wao.Ila ukweli utabaki kuwa Magufuli hakuwa fisadi,kinyume chake alichukia ufisadi wa aina yeyote.
Chuki dhidi ya Magufuli zilionekana hata ndani ya chama chake.Yeye kwa sababu ya utendaji wake uliotukuka, alikuwa hukumu tosha kwa viongozi wengine wababaishaji.Sitaficha ukweli kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2015,CCM ilikuwa njia panda,CCM ilikuwa inakaribia kuaga duru za kiasa za Tanzania.Kama chama, CCM ilijisahau,ikaweka maslahi ya wananchi pembeni na kukumbatia mafisadi wa aina zote na mabeberu.Mtizamo huu wa CCM ulifika kilele chake kwa kupitishwa Azimio Zanzibar, Azimio ambalo lilikumbatia ubepari na mafisadi moja kwa moja.
Hali ya wananchi kiuchumi iliendelea kuzorota,huku mafisadi na mabeberu wakiendelea kuneemeka.Tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho ikazidi kuongezeka,na vilio vya maskini vikasikika kila kona ya Tanzania.Ikawa dhahiri kwamba madiliko yalihitajika,tena kwa haraka,ili kubadili hali hiyo.Hata hivyo wanyonge hawakuwa na mtetezi na hali yao ikazidi kuwa mbaya.Uonevu wa kila aina ulionekana kila mahali,haki zikapotea.Mahakama badala ya kutoa haki kwa wananchi kikawa chombo cha kulinda mafisadi na na mabeberu,huku chombo hicho kikinyang'anya haki za wananchi.Jeshi la Polisi nalo likasimamia dhuluma,badala ya kusimamia haki na kulinda wananchi na mali zao.Badala yake wakalinda maovu kama uuzaji wa madawa ya kulevya na wizi.Polisi wakaogopwa badala ya kuwa kimbilio la wanyonge.Magereza yakajaa vibaka,na waliopaswa kuwepo magerezani wakawa mtaani wakistarehe, huku wakikebehi wananchi.
Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa uchaguzi Tanzania.Lakini kwa jinsi hali ya nchi ilivyokuwa,hapakuwa na shaka yeyote kwamba CCM ingepoteza uchaguzi ule na upinzani,specifically CHADEMA wangeingia Ikulu
Nilishasema hapo awali kwamba Magufuli alikuwa hukumu kwa viongozi wenzie kwa sababu ya umahiri wake katika utendaji.Niseme hapa pia kwamba wananchi walimkubali sana Magufuli,kwa sababu ya uaminifu wake na utendaji wake.Kwa bahati mbaya ndani ya CCM hapakuwa na kiongozi aliyekuwa na sifa zinazokubalika na wananchi,isipokuwa Magufuli,ingawa alikuwa hakubaliki sana ndani ya chama chake.Hii ikakilazimu chama kumchagua kupereusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa 2015.
Ni historia, sasa kwamba Magufuli alishinda katika uchaguzi ule.Baada ya ushindi wa kishindo na kusimikwa kuwa Rais,Magufuli alianza safari ya kuitengeza Tanzania mpya,safari ambayo sina shaka yeyote kwamba imemgharimu maisha yake.
Katika kuitengeneza Tanzania mpya,Magufuli alisimamia sera ya CCM kikamilifu,akaanzisha miradi mingi ambayo iliifanya Tanzania ipae kuichumi mara moja.Hii iliwezekana kwa kuwa kwanza yeye mwenyewe alikuwa mtendaji makini na mwaminifu.Hii ilimuwezesha kuunda serikali yenye watendaji waaminifu,makini na wenye weledi.Kwa hiyo kama nchi tukaweza kuongeza mapato kutoka Sh. Bil.800( tril.0.8) mpaka Tri.1.3! Fedha hii ikawa chachu ya maendeleo makubwa Tanzania kwa muda mfupi.
Niwakumbushe wasomaji wangu kwamba Magufuli ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza kuwa na ujasiri wa kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania ni tajiri.Wengine wote walijitahidi kuwa-aminisha Watanzania kwamba Tanzania ni nchi maskini.Hatua hii ilionyesha wazi kwamba Magufuli hakuwa na la kuficha na kwa hiyo alikuwa Rais na kiongozi mwaminifu.
Tabia yake ya uaminifu na kuwa a "no nonsense President," iliwafanya watendaji wote chini yake nao kutenda kwa umakini na uaminifu mkubwa.Matokeo yake Tanzania ikapata maendeleo kwa muda mfupi,akawa mfano ani na nje ya Tanzania.Magufuli akapata sifa kwa wananchi aliowaongoza,wakampenda na akapata sifa duniani kote.
Magufuli hayupo nasi tena,tunae Mama Samia Suluhu.Najua kwamba Magufuli sio Mama Samia,ila kama wananchi wa Tanzania,tunategemea utendaji uliotukuka kutoka kwake na hata zaidi.Tunajua the road ahead is bumpy and rough,kwa kuwa mazingira aliyokuwa nayo Hayati Rais Magufuli hayajabadilika na ina wezekana yakawa magumu zaidi.Hata hivyo tunategemea utumishi uliotukuka.
Ni lazima mmoja wetu afe kwa niaba ya wengi.Magufuli umekufa kwa niaba yetu,nenda kwa amani na kwa heri hero na jabali,kipenzi cha Watanzania na sisi tuko njiani.Karibu Mama Samia Suluhu.
Na inawezekana Sokoine alifanya yote aliyoyafanya Magufuli bila vituko visivyo na staha vya Magufuli.
Na wote wawili walikosea kwa kutaka kuongoza kibabe bila kuheshimu kanuni za msingi za uchumi.