Tanzania imewekewa mkakati maalum

Tanzania imewekewa mkakati maalum

Kuna nyeti bado hazijawa rasmi kwamba upo mkakati wa kijasusi wa kuingiza taifa hili kwenye maandamano makubwa very soon.

Mkakati huo unaundwa na majususi kutoka nchi mbalimbali za ulaya na amerika na several attempts zimefanyika kuwafanya wananchi walipuke
lakini imeshindikana. Sasa wanataka kutumia wanajeshi wetu. na attempts zao zinakua hivi:

1. wanaleta skendo (which is very true) ila wanangalia zile zenye impact kwa kundi kubwa la watu mathalani wanajeshi
2. Wanawatumia economic hitmen
3. Kuna crisis nyingine itatokea very soon kama ile ya mafuta then kabla haijaisha itatokea ingine in between wananchi wataingia barabarani
na hii ndio ntoleee either the government fall or situation changed.

Hiyo ndiyo brief niliyopata.

My TAKE: Ni kweli hali ya maisha ni ngumu, ni kweli tunao ufisadi na ni kweli viongozi wetu legelege. URANIUM itatuletea matatizo very soon.
kuna mapapa na manyangumi yanaililia lakini wataweza kuiexplore better when they have their own government.

Napenda sana kuona utawala wa ccm ukiondoka madarakani lakini sio kwa external forces but internal once.

Msiniulize source, sit down contemplate what is happening see what can be done to rescue.


Sio lazima upost kwenye hii thread cha msingi fikiria


Tanzania nchi yangu, Mungu ibariki Tanzania

Ndugu yangu naomba uelewe kuwa, haya mataifa interest yao siyo kuzipindua serikali zilizopo ktk nchi zenye rasilimali ulizozitaja, ukweli ni kwamba wanapindua nchi ambazo viongozi wake ni madhubuti kwa kutetea maslahi ya wananchi, na wanakataa mikataba ya kuwanyonya wananchi ikiwa ni pamoja na kukataa rushwa zao. Kwa Tanzania hilo haliwezi kutokea kwa kuwa viongozi wetu wanawasujudia hawa watu, na wanazidondoshea mate hela zao za rushwa huku kila mmoja akiomba mungu, wazungu waje na mkataba hadaa ambao yeye ni signatory ili asign na kupata Ten percent yake. Sasa ktk mazingira kama haya wataandaa maandamano ya nini wakati wanachokitaka wanakipata kiulaini tu wanapohitaji, tena kwa kusign mkataba wa Miaka MIA??

Ndugu yangu, nia ya hii post yako wewe unaijua, na hata sisi wana JF ni intelectuals tunaelewa, si wale wananchi mnaowaambia kuwa mkichagua upinzani basi kutatokea vita na wao wanaamini. Ninachotaka kukufahamisha ni kwamba kama maandamano yakitokea hapa nchini ni kwa sababu ya ugumu wa maisha uliopo na kukithiri kwa viwango vya rushwa na ubinafsi kwa watu tuliowapa dhamana ya kutuongoza, na si vinginevyo.
Kama ni gas, basi kuna nchi nyingi zenye gas nyingi kuliko Tanzania na Viongozi wake ni wagumu na hawahongeki kama TZ, nafikiri wangeshaanzia huko kabla ya kuja kwetu ambao viongozi ni kama Fisi wenye njaa ya RUSHWA. Vivyo hivyo kwa Gas na Uranium.

Kama ni maadamano wangekuwa wameyaandaa wangekuwa wamenyimwa kupatiwa madini yaliyopo TZ, lakini Kila kitu wameuziwa, kitu gani kitazuia wasiuziwe na hivi vingine.

Mimi nasema, tunatakiwa kuandamana sisi wenyewe ili kuzuia ushirikiano uliopo kati ya mataifa haya mumiani na viongozi wetu katika kutunyonya.
 
Back
Top Bottom