Tanzania Imefikaje Hapa na CCM Kutoa Maamuzi Yote ya Taifa? Ugaidi na Vitisho ni CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Imefikaje Hapa na CCM Kutoa Maamuzi Yote ya Taifa? Ugaidi na Vitisho ni CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by niweze, Jan 22, 2011.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania Imefikaje Hapa? Kuna makosa sisi kama Wananchi tumefanya kuweka watu kama hawa kuongoza Taifa letu. Kwanini tunaendelea kukubali sauti na maelekezo ya Chama kimoja wakati mfumo wa Siasa Tanzania ni Mfumo wa vyama vingi? Kutokana na Vitendo vya Kamati kuu ya CCM, Taifa zima la Tanzania lisikilize sauti ya hawa wala rushwa na wezi wa Taifa letu? Wananchi tumekataa na hakuna kusikiliza maamuzi ya CCM na Kamati zao.

  [​IMG]

  AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
  (1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja (hii ahadi ni sawa na vitendo vya Mugabe kwa wananchi wa Zimbabwe)
  (2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote (kama ni kweli Dowans na kuiba kura ni kumtumikia Nani? Kama sio Rostam na Mafisadi?)
  (3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma (kuna kitu CCM wamefanikiwa? Kipimo ni huduma za mahospitali muhimbili na hali za mashule)
  (4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa (CCM imeshinda kwenye rushwa? CCM ndio wala rushwa Tanzania na matunda ni utajiri wao na umaskini wa Watanzania?)
  (5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu (Kikwete na CCM vyeo ni dhamana na Faida kwani tunaona jinsi gani wanatumia Ofisi ya Raisi?)
  (6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote (elimi ipi CCM wanatumia kulitumikia Taifa? Elimu katika maamuzi ya kiuchumi Dowans na kuhesabu kura?)
  (7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu (CCM haishirikiani na watanzania wowote wale kujenga Taifa ni Ubinafsi mtupu na cover up after mess)
  (8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko (ukweli gani CCM umesema mpaka sasa? Dowans, EPA, au Richmond?)
  (9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika (CCM wanafanana na sera za Mugabe, Ben Ali, Mubarak, Museven, Kagame, Kibaki, Gabgo)
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hamna cha baraza la Mawaziri, bunge wala nini. Cc ndio imeamua kuwa kila kitu
   
 3. ketwas

  ketwas JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mwisho wao umefika kwani watasema kila kona,mimi sishangai kusikia tamko la mjumbe wa kata au wa kijiji akisema neno na likatelezwa,kila kona nimsemaji,wa serikali tunaenda wapi?waliokuwa wakidanganywa ni wale waliokuwa hawujui kusoma na kuandika enzi za mwalimu.na wakati wa mwalimu alikuwa anatumia busara sana sio kama hawa wa leo,wakae wakitambua,upepo ulioko dar ni sawa na upepo ulioko musoma,mbeya,mwanza nk
   
 4. S

  Shingo Senior Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nchi inaongozwa kwa proxy. Si vyombo halali vinavyojulikana kisheria vinavyofanya maamuzi. Wanaofanya maamuzi ni Magenge ya wahuni fulani wanaounganishwa na kitu kimoja tu; Madaraka. Vikao visivyo rasmi ndo huamua lipi lifanywe! Waliobaki mnaona wanakimbia kimbia hapa na pale na kusema hili na lile lakini ukweli nchi hii iko at our lowest point. Tukitoka salama, eeeh, sijui!
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naona kabisa hoja yako ilivyosimama!! Haiwezekani CCM kuendelea kuitolea taifa mitamko kwa kuendeleza utamaduni wao ule ule wa kipindi cha chama kimoja.

  Hata hivyo, enzi hizo bwana ukisikia Mchonga kaitisha kikao kikao kweli zi hizi karamu za mafisadi kugawana cha kunyoga hivi ambacho hata kabla hawajakimeza lazima wenyehaki tukairudishe upesi.

  Hivyo vitamko bora siku hizi wakaelezana tu faraghani wale wana CCM sugu watakaozikwa nayo hata akibakia mle mtu mmoja siku ya mwisho.
   
 6. V

  Vumbi Senior Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Haya yanamwisho siku siyo nyingi. Ila mimi nataka watanzania wateseke mpaka wale majani ili wafahamu CCM ni chama cha majambazi Uchaguzi mwingine ukifika watajua kuchagua viongozi wazuri.
   
 7. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  So stupid! that is how they are!!!!!!!!!!!!! Lakini sikio la kufa haliskii dawa ndio maana kelele zote zinazopigwa hawazisikii; na hii inaashiria kifo asilia cha serikali ya kidharimu ya CCM:kev:
   
Loading...