singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
RAIS wa Vietnam, Truong Tang San ameelezwa namna vijana wa Tanu, walivyoshiriki katika kuunga mkono jitihada za Chama cha Kikomunisti nchini, kupambana na ubeberu Marekani. Akiwa katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba, Rais San alielezwa hayo na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete.
Marekani ilipambana na Vietnam wakati ilipoingilia mzozo wa ndani wa nchi hiyo kutokana na watu wa Vietnam ya Kusini kutaka kujitenga na Vietnam ya Kaskazini mara tu baada ya Uhuru wa nchi hiyo mwaka 1945.
Akiwa na lengo la kuhakikisha Vietnam inabakia kuwa taifa moja, muasisi wa Uhuru wa taifa hilo, Rais wa Kwanza wa Vietnam, Ho Chi Minh aliongoza mapambano ya kuipiga Marekani na waasi wa Kusini, huku jeshi likiwa chini ya Meja Jenerali maarufu wa Vietnam, Giap Nguyen na kufanikiwa kuwasambaratisha wa Marekani.
Kikwete alikumbusha kuwa kutokana na mapambano hayo, vijana wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu walikuwa wakichanga fedha ili kukisaidia chama cha Kikomunisti, na mmoja wa vijana waliokuwa wanapewa fedha za michango ili kuziwasilisha maeneo husika alikuwa Benjamin Mkapa.
“Kama mnavyojua hivi sasa Rais San ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam. Kitendo cha kufika hapa leo (jana) kinadhihirisha namna Vietnam na watu wake wanavyotambua na kuheshimu kazi kubwa iliyofanywa na CCM katika kulipigania taifa lao.
“Hatua hii itaendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kwa nchi zetu mbili na hasa Tanzania ambayo inapigana kuingia katika uchumi wa kati, huku Vietnam ikiwa na uchumi wa kwanza,” alisema Kikwete.
Awali, alipowasili katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, Rais San badala ya kuingia ndani, alizungumza kwa muda na mwenyeji wake, Mwenyekiti Kikwete na kuamua kuvuka upande wa pili wa barabara ili kuwasalimia wanachama wa CCM waliokuwa wamejipanga kumlaki kiongozi huyo.
Hata hivyo, Rais huyo wa Vietnam hakuweza kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ofisi hizo za CCM kutokana na kuwa na ratiba nyingine ya kwenda kwenye mkutano wa biashara baina ya Tanzania na Vietnam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.