Siasa za Ujamaa zilituathiri sana mpaka leo

Siasa za Ujamaa zilituathiri sana mpaka leo

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,674
Reaction score
14,097
Hizi siasa za ujamaa/ukomunisti huwa ni mbaya sana pale unapo pata viongozi waroho.

Siasa za kijamaa au kikomunisti ni nzuri sana kwa kuzisoma lakini ni mbaya sana pale zinapokuwa zinatekelezwa hasa kwa kuzingatia sisi watu hatujakamilika.

Hizi siasa tulipaswa kuwaachia wachina huko huko tulipo wakopa kwetu ziligeuka laana mpaka leo.

Ubaya mkubwa hizi siasa za kikomunisti ni chama kumeza kila kitu ndani ya nchi na hichi ndicho kinacho tumaliza hapa Tanzania.

Mifumo yote hapa nchini imemezwa na chama sio mifumo ya haki, sio majeshi sio chochote.

Chama na viongozi wake wanaweza amrisha lolote litendeke na likatendeka hakuna mahali kutakuwa na pingamizi.

Hizi siasa zimetugeuza wakimbizi na watumwa katika nchi yetu wenyewe.

Ilikuwa ni disaster kubwa Nyerere kutuletea hizi siasa za kipuuzi.

Siasa hizi za kipuuzi mwenyekiti wa CCM ni Mungu wa nchi kwa wale wafuasi wa dini nafikiri mnaelewa naposema Mungu namaanisha nini kwenu.

Toka kwa Nyerere mpaka sasa hakuna anayekohoa mbele ya mwenyekiti wa CCM hakuna hata mfumo wowote utakao jaribu kohoa kwake ukabaki salama.

Ndani ya nchi za kikomunisti chama ndio kila kitu na kinaendesha na kuamua kila kitu.

Ulikuwa upumbavu sisi kupokea aina hii ya siasa za kipuuzi.

Kinacho wasaidia hao wachina, wa Vietnam kidogo wao wana viongozi wenye akili licha ujinga wa siasa za kikomunisti lakini hawaachi kujali watu wao na maendeleo ya nchi yao.

Sisi huku tumejikita kwenye kutawala zaidi na kulinda chama na sio maslahi ya nchi na watu wake.

Itahitajika nguvu kubwa sisi kujitoa katika aina hii ya siasa za kipuuzi za kikomunisti.

Yale mabadiliko ya Mwinyi ya 1992 na 1995 yalikuwa ya kitapeli lakini ukweli halisi hali bado ipo vile vile.
 
Tofauti ya viongozi wetu na wa wenzetu.

Wa kweetu
ni walafi, wao kwanza, kizazi kijacho kitajijua chenyewe, maslahi kwanza, taifa itaambuliaga chochote, kwanza ni 10% yake kisha memgine yatafata hata kama taifa linapigwa hajali hiyo

Wenzetu
Taifa kwanza, maslahi binafsi yanafata, kwenye deal wanaangalia taifa litafaidika vipi kisha nae anaangalia namna ya kupiga.
 
Mifumo yote hapa nchini imemezwa na chama sio mifumo ya haki, sio majeshi sio chochote.

Chama na viongozi wake wanaweza amrisha lolote litendeke na likatendeka hakuna mahali kutakuwa na pingamiz
Mkuu ni suala la muda tu, kuna siku utando huu wa madaraka utakuja kukatika.

**Al Bashir wa Sudan aliunganisha chama na dola kikweli kweli, lkn alitolewa kwa maandamano.
**Gadaffi aliishika nchi ikawa chini ya familia yake, hata kufikia kuwaita raia wake cockroaches (mende), rats (panya), n.k. Lkn aliondolewa.

CCM ikiendelea kukaza fuvu, mitano ijayo haitaisha, kitanuka.
 
Ieleweke Ujamaa sio Ukomunisti.

Itoshe kusema Mwalimu Nyerere aliukataa Ukomunisti, na wala Tanzania haijawai kuwa na sera za kikomunisti.

Mleta mada ni mpotoshaji(misleading). Hajui hata maana halisi ya Ujamaa na kama anajua, anapotosha kwa makusudi. Alaaniwe kwa nguvu zote.
 
Tatizo siyo siasa, ni watu na uwezo wao wa kufikiri kwa asilimia kubwa.

Siasa ya ujamaa haifundishi kuachia wageni njia kuu za uchumi, kuruhusu wachache kujilimbikizia mali huku wengi wakiteseka (inazuia kujilimbikizia mali kwa wachache na kuhimiza uzalendo na kulinda mali za uma). Sasa, hivi hakuna ujamaa bali kuna uzuzu wa halaiki.

Kuna vyama vingi (kila raia ana Uhuru wa kujiunga kokote) , ndani ya chama tawala kuna kupambana kwa hoja hata kwa mizengwe (Mpina, Bashe/serikali na sukari), Uhuru wa habari hata kama vyombo vinaandika kwa uelekeo mmoja (tatizo watu).
 
Ieleweke Ujamaa sio Ukomunisti.

Itoshe kusema Mwalimu Nyerere aliukataa Ukomunisti, na wala Tanzania haijawai kuwa na sera za kikomunisti.

Mleta mada ni mpotoshaji(misleading). Hajui hata maana halisi ya Ujamaa na kama anajua, anapotosha kwa makusudi. Alaaniwe kwa nguvu zote.
Ujamaa ni mtoto wa kwanza wa ukomonist .


Mzee Nyerere alicopy kila kitu cha ukomonist.

Kuanzia bendera. Alibadili mundu na kuweka jembe

Azimio la arusha

Uporaji wa nyumba.

Nguo zake

Na kuwalazimisha wenye dini wote wajiajiriwa ktk ofisi za umma wafate imani ya Ujamaa kwa maana ukana Mungu, ukana dini.

Kwa ufupi imani ya Ujamaa ni laana
 
Ieleweke Ujamaa sio Ukomunisti.

Itoshe kusema Mwalimu Nyerere aliukataa Ukomunisti, na wala Tanzania haijawai kuwa na sera za kikomunisti.

Mleta mada ni mpotoshaji(misleading). Hajui hata maana halisi ya Ujamaa na kama anajua, anapotosha kwa makusudi. Alaaniwe kwa nguvu zote.
Ni ngumu kuutenga ukomunisti na ujamaa.

Ukomunisti na ujamaa unaenda sambamba ni sehemu ndogo tu unaleta tofauti.

Baada ya ziara ya Nyerere China ndio iliyokuja kusimika fikra za kikomunisti komunisti Tanganyika na Nyerere alivutiwa zaidi na yale aliyo shuhudia China ya Mao.

Mwalimu asingeweza kuwa kama mkomunisti Mao kwa sababu ukomunisti ule wa China ungegusa mpaka masuala ya imani yake jambo ambalo
kwake lingekuwa gumu.

Mwalimu Nyerere alizihusudu sana fikra za kikomunisti na ndivyo ilivyokuwa TANU,CCM

Aliuhusudu ukomunisti hasa wa China akataka kuupaka rangi na kuuita ujamaa wa Afrika.
 
Ndani ya nchi za kikomunisti chama ndio kila kitu na kinaendesha na kuamua kila kitu.
Pengine katika yote uliyo andika ni hili pekee ndilo umejitahidi kuliweka sawa, mengine yote ni uchafu mtupu.

Sasa mimi nakueleza hivi: nchi kama Tanzania hii, yenye baadhi ya watu wanaoonekana kuwa kama misukule kama wewe hapo, inafaa ipate, siyo "chama" kama ulivyo kielezea hapo kwenye huo mstari; bali inahitajika DIKTETA hasa, pengine hata kumshinda Magufuli katika baadhi ya mambo. Hapana, siyo Dikteta anayeua na kuumiza watu hovyo hovyo tu; bali dikteta asiyevumilia ujinga kama huu unaojaribu kutetea humu. Dikteta asiyevumilia mafisadi na takataka zozote zile.
Jambo la muhimu kwa dikteta huyu, liwe ni kufuata sheria zilizopo, na matakwa ya Katiba tu basi.

Mengine yooote, ya kiswahili kireeefu na stori kama hizi zako zinazoonekana hujui unachokieleza, upuuzi wa namna hiyo dikteta huyo anaushughulikia ipasavyo bila ya huruma, lakini bila kuonea au kupendelea mtu.
Huko maofisini mnakoshinda kutwa mkipiga stori za aina hii, mnakomeshwa.
Dikteta huyu tukimpata, angalau kwa mika kumi tu, nchi hii itanyooka vizuri kabisa..

Mkuu ''Mto nikwambie wazi, huna unalojua katika hayo yote unatojaribu kuyaeleza kwenye vi-mada choka hivi unavyo anzisha JF.'
 
Ujamaa ni mtoto wa kwanza wa ukomonist .
Sio kweli hata kidogo. Mnapotosha Ujamaa wa Nyerere.

Hata Capitalism mtoto wake wa kati ni Ujamaa. Bismarkism. Jiridhie.
Mzee Nyerere alicopy kila kitu cha ukomonist.
Sii kweli hata kidogo pia. Nyerere alikuwa na falsafa ya kipekee. Sio kweli alicopy kutoka kwa wakomunisti. Sasa acopy halafu ajiunge na Non Aligned Movement?
Kuanzia bendera. Alibadili mundu na kuweka jembe
Kubadili bendera hakukufanyi uwe Mkomunisti.
Azimio la arusha
Umelisoma? Azimio la Arusha lilisema tuwe Wakomunisti?
Uporaji wa nyumba.
Aliwapora kina nani? Kwa sababu zipi?
Nguo zake
Ha ha.
Na kuwalazimisha wenye dini wote wajiajiriwa ktk ofisi za umma wafate imani ya Ujamaa kwa maana ukana Mungu, ukana dini.
Sio kweli-Waafrika have been religious before.

Wazungu, Waarabu ndio waliotaka tuukane dini zetu na Mungu wetu.

Nyerere alitaka kama walivyotaka Waingereza. Separation of Church and State. Usipotoshe na kugeuza ukweli.
Kwa ufupi imani ya Ujamaa ni laana
Sio kweli hata Kidogo.

Mtu wa Kwanza kuleta Ujamaa alikuwa ni Mjerumani.

Rejea Bismarkism. Utaelewa.

Socialist agendas ama ideology mpaka leo hii zipo Norway, Sweden Finland etc.. Itoshe kusema hata hii Capitalist system isingewezekana kama sio kwa mgongo wa Socialism. Marekani is embracing Socialism today.

Wacha hizo propaganda na upotoshaji -you're misleading.

Ujamaa sii laana, umejitungia tu hayo maneno.

Nordic countries zipo na Ujamaa. Zimelaanika kivipi? Capitalism ndio Ushetani wa Juu kabisa🤡🙌🏾
 
Ukiangalia hata nyuso zao wala sio wajamaa ni majizi unakuta jitu limevimbiana halieleweki wapi ni wapi yoote hayo ni madhara ya ulafi mwisho wa siku yanaishia visukari na ma presha
 
Ieleweke Ujamaa sio Ukomunisti.

Itoshe kusema Mwalimu Nyerere aliukataa Ukomunisti, na wala Tanzania haijawai kuwa na sera za kikomunisti.

Mleta mada ni mpotoshaji(misleading). Hajui hata maana halisi ya Ujamaa na kama anajua, anapotosha kwa makusudi. Alaaniwe kwa nguvu zote.
Trying to separate Ujamaa from Ukomunisti is as futile as trying to separate Mickey Mouse from Walt Disney. You simply can't, no matter how hard you'll try.

And truth be told Babu Nyerere was a hardcore Marxist-Leninist-Moist. I even remember listening to him flaunting the idea of being close to Chairman Mao, and imploring the TZ establishment to emulate Deng's economic reforms.

Him morphing from a humble and devout Western European Fabian Socialist into a hardcore Eastern Europe Marxist Leninist was a startling and appalling even to his acolytes like Harold Wilson and James Callaghan.​
 
Back
Top Bottom