Tanzania hii:kila waziri shangingi gx v8 jipyaaa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania hii:kila waziri shangingi gx v8 jipyaaa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tonge, Nov 29, 2010.

 1. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WAKATI mawaziri na manaibu wawaziri wakikabidhiwa magari mapya, baada ya kuapishwa Jumamosi iliyopita, serikali imeibuka na kusema sio mapya ni ya zamani.

  Kauli hiyo inaibua utata kutokana na kuwa baada ya kuapishwa viwanja vya Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, kila waziri alikabidhiwa dereva mpya na gari jipya aina ya Toyota GX V8, badala ya gari aina ya Toyota VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na mawaziri waliopita.

  Ununuzi wa Toyota GX V8 mpya, unashiria serikali bado haijawa tayari kuunga mkono msimamo wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye amekuwa akisikika akitaka kusitishwa ununuzi wa magari ya kifahari ili kupunguza matumizi ndani ya serikali.

  Toyota GX V8 moja huuzwa kati ya Sh210 milioni hadi Sh240 milioni, hukuToyota VX V8 moja inauzwa sio chini ya Sh180 milioni.
  Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, alisema magari hayo sio mapya na kwamba, yaliyotumiwa na mawaziri waliopita.
  Rais Jakaya Kikwete ameigawanya iliyokuwa Wizara ya Miundombinu na kuwa wizara mbili; Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.

  “Yale magari sio mapya, yalikuwepo. Kwanza uliyaona au unasema tu, hamjayachunguza vizuri jamani, fanyeni uchunguzi,’’ alisema Chambo na kukata simu.
  Mawaziri wote na baadhi ya manaibu walikabidhiwa magari hayo (GX V8), huku manaibu wengine wakikabidhiwa VX V8.
  Sababu ya baadhi ya manaibu mawaziri kukabidhiwa VX V8 badala ya GX V8, ni kutokana na kutokamilishwa kwa taratibu za kutokamilika.

  Mmoja wa manaibu mawaziri (jina tunalo), alikabidhiwa VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi, John Magufuli, ambaye sasa ni Waziri wa Ujenzi.

  Gazeti moja la kila siku (si Mwananchi) limeeleza kuwa ununuzi wa magari hayo, umegharimu serikali Sh9.3 bilioni na kwamba, takwimu za iliyokuwa Wizara ya Miundombinu zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2005/06 magari makubwa ya kifahari yapatayo 6,000 yalikuwa yamenunuliwa na serikali kwa gharama inayokadiriwa kufikia Sh160 bilioni.

  Miongoni mwa magari hayo ni Toyota Land Cruiser (VX/ GX V8, Prado) yapatayo 1,655, Nissan Patrol na Land Cruiser 885, Mitsubishi Pajero 400 na mengineyo.

  Tangu kipindi cha serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kumekuwepo na mjadala kuhusu matumizi makubwa ya serikali hasa katika ununuzi wa magari ya kifahari kutokana na kuendeshwa kwa gharama kubwa.

  Source MWANANCHI ya Leo.

  Wadau wengi wanataka viongozi watumie magari ya kawaida kama ilivyo kwa nchi ya Kenya na Rwanda.Tena gari yenyewe ni ya kutokea Mbezi kwenda Posta kwa ofisi, safari nyingi za mikoani anatumia ndege na chache hio GX V8.

  Hao ni mawaziri tu bado makatibu wakuu, wakuu wa vitengo wizarani, wakurugenzi wa idara tofauti n.k huku hakuna madawa hospitalini, maji vijijini, shule chakavu na walimu hamna, barabara mbovu na hali ya mTZ ni duni kuliko maelezo.

  Je tutafika kweliiiiiiiiiiiiiiiiii?
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  :redfaces:
   
 3. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  so painful
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tukishanunua hizo vx na gx tusihofu sana serikali ya japan itatujengea matundu 16 ya choo kwenye mashule yetu
   
 5. D

  Dina JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Yale yaleeee.......halafu mnasema elimu ya bure haiwezekani!
   
 6. M

  Matarese JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kama mtakumbuka vizuri ilishawahi kusemwa kwamba sh. bilioni 160 zinatosha kuwapa mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu kwa asilimia 100 kwa mwaka mmoja.
   
 7. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii nimeipenda. Ndiyo upeo wetu wa kufikiri watanzania. Inasikitisha kwa kweli.
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  "Kwanini Tanzania ni masikini?"
  "SIJUI"
   
 9. sholwe

  sholwe Member

  #9
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini watanzania ni masikini, "even me! i don't know" ...
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wala siyo shida, subiri mama zetu wajawazito waletewe bajaj kama ambulance!
   
 11. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mtoto wa mkulima anatakua anatoa Mil.10 kila mwaka mpk pale cheo chake kitakapokoma huku yeye anacruz road na V8 la mil.220 hapo hapo wanasema mkopo asilimia mia kwa wanafunzi wote haiwezekani.......Sasa hapa mi nina uhakika mtoto wa farmer atachomoa kuyapanda haya magari yeye ataomba serikali impe Mandolini awe anafanyia shughuli za serikali....................

  220m * 28 = 6.16 billions

  160m * 22 = 3.52 Billions

  total 9.68 Billions

  Hii ni gharama ya usafiri wa mawaziri hapo mchomoe Rais, Waziri Mkuu na makamu wa Rais. hapo hujaweka gharama za uendeshaji wa hii MIKOKO ya adabu.....kama wese, Service, tires etc. Sijui watakua wanatumia shilingi ngapi tu kwa mwaka hawa jamaa.....Wanakula bata kinyama huku sisi tunazidi kutaabika kinyama........................YANA MWISHO.......
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwamba ni mapya au siyo mapya siyo hoja. kwa nini wanatembelea magari ya ghali hivyo na wakati serikali haina pesa za kuhudumia wananchi wake? kikwete alipoahidi kubana matumizi alikusudia kubana matumizi yapi?
   
 13. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hizi pesa hazitoshi kugharamia elimu ya bure kwa mwaka mmoja?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Kuelewa tu tumetoka wapi...
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,548
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  "Tanzania ni nchi masikini kwa sababu haina hela" JK
   
Loading...