Euphransia
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 937
- 778
Bajeti ya 2016/2017 ya trioni 29.5 mpaka sasa imebaki miezi 3 hatuoni ilivyotumika wala serikali haitaki kuizungumzia wachumi wetu wamekaa kimya.Jana Waziri wa Fedha anatangaza kuwa bajeti ya 2017/2018 itakuwa ya trioni 31.6 hakika nashindwa kuelewa kwani viongozi wetu wanakuwa sio wakweli.Nilitegemea tungeelezwa utekelezaji wa bajeti iliyopita tulifanikiwa kiasi gani tulikwama wapi .Watanzania wa Leo sio wa miaka ile tunauelewa mkubwa wa uchumi kuliko viongozi wa serikali wanavyofikiria.