Tanzania hatuna sera mama

status quo

Member
May 6, 2011
87
38
ukienda marekani utasikia conservatives (right wing) na liberals(left wing), ukienda uingereza tories(right wing conservatives) na labour(left wing), ukienda kenya PNU(right wing) na ODM(left wing), nk.... lakini hapa kwetu kila siku ufisadi, posho, hatuna direction hatujui hata chama kilichoko madarakani kinatekeleza sera gani , mara utasikia ujamaa, wengine ubepari kipi ni kipi. na hili ndilo tatizo linaloisumbua nchi yetu leo hii kama chama kilichoko madarakani kingekuwa kinatekeleza sera ya ubepari basi hiyo nyongeza ya posho tusinge ipigia kelele, lakini kwa sababu tulivyo wachagua hawakutuambia juu ya sera yao ndio maaana kuna kelele kila pande ya nchi juu ya posho hizo. nchi inaendeshwa kwa ahadi tu, wapi na wapi. ndio maana na thubutu kusema tanzania tumepoteza mwelekeo.
 
Kwa lugha nyepesi Hatuna "National Ideology" yaani ukiwachukua hata mawaziri watano kutoka wizara tofauti ukawauliza hivi tanzania tunaelekea wapi tegemea kupata majibu tofauti kabisa.nini wananchi wa kawaida huko tegemea kusikia mi CCM or CDM or simba or Yanga.

In 20 plus years back Malaysia walikuwa wapo nyuma sana kimaendeleo walihamua kuwa"National Ideology" yao ambayo kila mtu alikuwa anaplay role toward that "Ideology" na matokeo yake yameonekana.Hii kila mtu kuimba wimbo wake hakitupeleki popote.
Mpango Mkakati wa miaka mitano ulizinduliwa dodoma hautaweza kutupeleka popote kama haitakuwa na "National Ideology" regardless of Dini,Kabila au Chama wote tunashiriki kila mtu kwa nafasi yake kuitransform Tanzania kuelekea kule tunakotaka.

Lakini leo tuulizane hapa ushiriki wetu kwenye hata huo Mpango mkakati wa nchi ni nini?au huo Mpango Mkakati ni wa viongozi tu?

Mytake: Tanzania aiweze kuwa endelea kwa kufanya vitu kwa mazoe na kwa sytle ya do things on your own syndrome "
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom