Tanzania hatuna mungu? Mungu anawaona mjue | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania hatuna mungu? Mungu anawaona mjue

Discussion in 'Great Thinkers' started by Dotto C. Rangimoto, Sep 15, 2016.

 1. Dotto C. Rangimoto

  Dotto C. Rangimoto Verified User

  #1
  Sep 15, 2016
  Joined: Nov 22, 2012
  Messages: 1,964
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  papapapapapapa.jpg

  Tanzania hatuna Mungu kama taifa? Nianze mada yangu na swali hilo la uchokozi.

  Kuna kamtindo kamezuka mtandaoni, mtu ataandika ya kuandika kisha anahitimisha kwa "mungu anakuona" , na sasa imeanza kusambaa ujumbe wa kuonya watu wasitaje jina Mungu bure. Hii ikapelekea nijiulize na kutafakari, jina la Mungu yupi? na hilo jina lipi?

  Katika tafakuri yangu, nikagundua asili ya onyo hili ni andiko kutoka kitabu cha biblia na onyo hilo ni moja kati ya amri kumi za Mungu.

  "Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure."

  Kutoka 20:7

  Ooh, kumbe amri na agizo hili lina wahusu watu wanao amini au kumfuata Mungu wa Biblia. Hao ndio hasa andiko na agizo hili linawahusu. Kumbuka hapo juu ya katika maswali ya kichokozi mada nilijiuliza Mungu yupi? Na sasa jawabu ni dhahiri ni Mungu wa Biblia au Mungu wa Mussa.

  Kwahivyo, hawa wanao sambaza ujumbe kuwa "msilitaje bure jina wa Mungu" bora wangelenga ujumbe wao kwa wahusika badala ya ujumbe huo kuwa wa kijumla zaidi. Namaanisha ujumbe huo ungewalenga wale wanaomini na kumfuata Mungu wa Mussa. Kwavyovyote vile watu hao ni wakristo.

  Hata hivyo, panaweza kuibuka hoja, kuwa Mungu ni mmoja na ya kwamba mungu ni mungu tu na ujumbe huo unawalenga watu wote. Hoja hii sio sahihi na inakosa pa kuegemea, na hasa ukizingatia Mungu si mmoja, hakuwahi kuwa mmoja na kamwe hata kuwa mmoja.

  Hili linaelezwa vizuri na Mungu wa biblia kupitia vinywa vya manabii wake kwa nyakati tafauti.

  "Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la Bwana, Mungu wetu, milele na milele."
  Mika 4:5

  Mungu kupitia kinywa cha nabii Mika, anatumbia kila taifa na kila kabila lina Mungu wake, na si Mungu tu, bali kila huyo Mungu ana jina lake. Kwahivyo kama vile taifa la Israeli lilivyokuwa na Mungu wake, kwavyovyote vile na ndivyo ilivyo taifa la Tanzania lina Mungu wake.

  Ajabu sana, mtu akila maharage yake ya Mgeta tena yale mekundu yenye gesi kwelikweli, kashiba alafu anasambaza ujumbe wa Mungu wa Israeli kwa watanzania alafu akitaraji sisi tuuheshimu huo ujumbe kama vile Tanzania au watanzania hawana Mungu kama taifa.

  "Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu wakasema, Maneno haya ni mazuri"

  1 Wafalme 18:24

  Kila Mungu hujifanya ana nguvu kuliko mwingine au wengine, kwahivyo hata Mungu wa Israeli pamoja na kwamba anatambua wapo miungu mingine, yaani hayuko peke yake, lakini kama ilivyo kwa Miungu mingine, Mungu wa Israeli hutamba na hujigamba yeye ndio zaidi. Si hoja yangu wala mada yangu kujadili nguvu na udhaifu wa Mungu wa Israeli, hoja wangu ni kuwa hayuko mwenyewe.

  JINA LA MUNGU WA ISRAELI.

  Huko juu nilisema kuwa ile amri ya "usilitaje jina la Mungu bure" nilisema ni agizo au amri ya Mungu wa Israeli kwa wana waisraeli. Amri hiyo katika kitabu cha kutoka 20:7 inakataza jina la Mungu wa Israeli lisitajwe bure, lakini hilo jina lipi?

  Ukisoma vizuri andiko hilo, utagundua fika kuwa hawajakatazwa kutamka neno "Mungu" bure bali wamekatazwa kutaja "jina" la Mungu bure. Hilo "jina" ni lipi hasa?

  Kwa mujibu maandiko mbalimbali ya biblia, na wenye kujua, Mungu wa Israeli alijidhirisha kwa majina tafauti kwa manabii tafauti na kwa wakati tafauti. Na kila nabii alimwita Mungu wa Israeli kwa jina lake.

  "Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote"

  Zaburi 83:18

  Mungu Israeli alijihidhirisha kwa Daud kwa jina la YEHOVA, kwahivyo na asilimi kubwa ya manabii kabla ya kuja kwa Yesu Kristo, Mungu wa Israeli alijidhirisha kwao kwa jina la 'YEHOVA. Kwahivyo walivyo ambiwa wasitaje jina la Mungu wao bure ilimaanisha wasitamke neno "YEHOVA" bila sababu za msingi(usilitaje bure)

  Enzi za Yesu Kristo.

  Asilimia kubwa ya wakristo isipokuwa wasabato na mashahidi wa wa Yehova, hawafuati au hawayapi umuhimu au uzito mkubwa mafundisho ya manabii waliokuja kabla ya YESU, wao wanayaita mafunzo hayo ni agano la kale, na ya kwamba sasa ni zama mpya, zama za Yesu, naam, ni zama za AGANO JIPYA.

  Wao wanafuata mafundisho na maagizo ya Yesu Kristo tu. Kwahiyo, kama wao nao wanafuata hili agizo la kutotaja jina la Mungu wa Israeli bure, basi ni wazi lipo jina alilo wafundisha YESU kuwa ndio jina la Mungu, na jina hilo hawatakiwi kulitaja bure. Je, Yesu aliwafundisha au kuwatajia wakristo jina la Mungu?

  Jawabu ndio, rejea aya hii.

  "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. JINA LAKO nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu.."

  Yohana 17:3-6

  Hapa Yesu Kristo anatuambia kuwa JINA LA MNGU amewadhihirishia wanafunzi wake na watu wanao mfuata. Hilo jina Mungu alilowatajia ndio wanatakina wasilitaje bure, wakilitaja wawe na sababu za msingi kabisa za kulitaja.

  Wasambaza ujumbe ule, wasiishie kusambaza tu kuwa wakristo wasitaje jina la Mungu Bure, bali walitaje hilo jina la MUNGU. Na ili niamini kuwa wakristo ni wafuasi wa Yesu Krsito kwelikweli na ya kwamba si waigizaji au maamluki wa shetani, leo waje hapa waniambie, JINA LA MUNGU walilofundishwa na YESU ni lipi? Walitaje, kama Daud alivyolitaja jina Mungu alilofundishwa na Mungu enzi zake kuwa ni YEHOVA.

  Namaanisha wasome BIBLIA kuanzia mwanzo hadi ufunuo, kisha watutajie ni wapi Yesu kafundisha au kawatajia jina la Mungu kama alivyo dhihirishiwa, wakikosa ina maanisha wapo wanafunzi wa Yesu na wapo wafuasi wake wanaomjua zaidi Yesu kuliko wakristo na hao ndio wenye kulijua jina hilo na hao ndio hasa wanafunzi wa Yesu, na hao ndio walio ambiwa wasilitaje jina la Mungu wa Yesu na wa Israeli bure, sio wewe mchaga wa Kibororoni unajitia kilanga cha ngeda cha kuacha kubeba mwana ukabeba bwana! Umeacha uafrika wako na kubeba vya wageni kwa mikono miwili.

  MWISHO.

  Wewe utakaye tukana baada ya kusoma haya, au wewe utakaye tafakari baada ya kusoma haya, fahamu Mungu waTanzania anakuona. Wataka kulijua jina lake? Muulize Lowassa.

  Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
  Call/whatspp 0622845394 Morogoro.
   
Loading...