Tanzania haiwezi kuendelea kwa mfumo wa sasa serikali inafanya mambo mengi sana!!!!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,607
8,744
Tatizo kubwa la Tanzania sasa hivi ni kwamba kila kitu muhimu Tanzania kinafanywa na serikali. Huu mfumo si mzuri kwa nchi na kama nchi siyo ya madicteta huu mfumo hauwezi kufanikiwa. Serikali ya Tanzania inashughulikia mfano vibali vyote vya viwanja Tanzania, barabara zote Tanzania, Hospitali zote ndogo hasa za vijijini Tanzania, walimu karibu wote wa Primary school na baadhi ya sekondari, wanavyuo na mikopo, wizara na idara za kusambaza maji Tanzania nzima, shirika la umeme Tanzania nzima (Tanesco), Shirika la Ndege Tanzania, Polisi wote na jeshi, wabunge wote wa Bara, visiwani na wawakilishi, mabalozi wote n.k. Hii ndiyo sababu kubwa Tanzania haiendelei kwani hakuna serikali ya kidemocrasia inaweza kumiliki shughuli nyingi hivyo. Badala ya wananchi kuhitaji serikali kubwa wananchi wanatakiwa kuhitaji serikali ndogo ambayo inafanya vitu muhimu tu ambavyo wananchi wenyewe hawawezi kufanya.Bila kufanya hivyo hatutaweza kupunguza rushwa kwani wafanyakazi ambao wanategemewa kwenye mtandao wa mishahara na vibali ni serikali.
Siwezi kutoa plan nzima lakini baadhi ya sehemu nitatoa mifano.

1. Tanesco inaweza kuvunjwa kwenye makundi matatu na kupunguza umuhimu wa kuwa na serikali kwenye hili
2. ATC ifutwe kabisa haina sababu na ni kitengo cha watu kutafutia rushwa. Kampuni ina ndege 2 au tatu lakini wafanyakazi na madeni mengi je inasaidia nini nchi. serikali ingetakiwa kusaidia sekta binafsi kufanya hii biashara na hiyo itaongeza ushindani.
3. Hospitali: serikali inatakiwa kuruhusu clinics za kisasa za kibinafsi ili kupunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa matibabu. Mfano serikali inatakiwa kuruhusu Mobile Hospital hasa vijijini kwani madoctor wengi hawawezi kwenda kukaa vijijini na hatuna madoctor wa kutosha kukaa vijiji vyote hivyo Mobile Hospital ni madoctor kutembea vijijini kama team na kuweka kemp ya matibabu kwa siku chache na kwenda kwenye kijiji kingine. Serikali iruhusu zaidi watanzania wa kawaida kufungua Imaging places kama za X-rays, CT Scan, Therapy baada ya ajali, Diabetic places n.k watu wa kawaida wafanye kama biashara kwani hatutaweza kuwa na hizo hospitali za rufaa kila mahali na zifanye kila kitu!!!. Hii pia itapunguza migomo kwani waajiri watakuwa watu binafsi.
3. Kutafutwe suluhu ya vibali vya viwanja, je ni kwa nini vibali vya viwanja vichukue miaka kupata wakati una kila kitu?
 
Back
Top Bottom