mikopo inatolewa kwa vijana wote bila kujali chuo ni public au private.ndugu zangu wa jf;
kwanini vyuo vya umma tu? Ina maana vyuo vingine, binafsi, havifaidiki na bodi ya mkopo? Why? Kwani huko tumaini hakuna maskini? Au ndio yaleyale, myths, ya zamani?
Je watanzania tungekuwa wa kweli, wakati wa ujazaji wa form za mkopo haya yote yangetokea? Je kuficha ukweli, hasa wa vipato vyetu, ndio tatizo?
mikopo inatolewa kwa vijana wote bila kujali chuo ni public au private.
Mimi naona we have a problem kwa sababu hapa tuna mafungu mawili ya wanafunzi/wazazi.Fungu la kwanza ni la kina sisi hoe yakhe na la pili ni la wenye nazo.Unapofunga chuo wote wanaumia waliojilipia na wanaosoma kwa mikopo.Suluhisho lipo, mzazi mwenye uwezo amlipie mwanae asiye nao alipiwe hata 100% .Njia rahisi ya ku control hii ni ku publish kwenye magazeti orodha ya wanafunzi WOTE waliopitishwa kupewa mikopo,anwani zao na za wazazi/walezi wao kisha umma wa watanzania upewe fursa ya kutoa pingamizi kwa siri.Watanzania tunajuana, atakayesema mzazi wake ni lofa wakati zimemtembelea umma utamuumbua,na adhabu ya ku cheat iwe ni kifungo bila faini,akifungwa mzazi mmoja/mtoto mmoja wengine tutashika adabu.TRA wahusishwe maana vibopa wote wa nchi hii wana TIN number.Mambo ya pangu pakavu tia mchuzi tuachane nayo.mnasemaje wadau?
1. Hivi utoaji Vitambulisho vya taifa vimefikia wapi?
2. Kumekuwepo na oungo..ktk ujazaji wa hizi form...kutambua nani maskini na yupi anauwezo. Huu ni utamaduni mbaya wa kusema uongo na kupeta tu bila kuchukuliwa hatua za sheria!
Waliodanganya waainishwe na kuchukuliwa hatua!
Mkuu hii hesabu ya kwamba zinahitajika Ths Bilioni 1200 unaweza kusubstantiate or else kuelezea source maana sijawahi kuisikia mahali pengine.
Pitia mjadala vizuri utakuta page ambayo nimederive hiyo billion 1200.
Mfano wa Cuna hauendani na mjadala wa wanafunzi wa Tanzania , kwa sababa Cuba wanafunzi wanasoma bila kulipa ada, lakini hawapewi pesa ya chakula wala pesa ya accomodation. Utaratibu huu unatumiwa na nchi nyingi tu za Ulaya. Wanafunzi wa Tanzania wanataka kupewa aslimia 100 ya mahitaji yao na siyo asilimia 100 ya ada.
Nadhani cha kufanyika ni kubadilisha sera kidogo na kusema utaratibu wa kuwapa wanafunzi posho ya chakula, malazi, vitabu na stationary ufutwe ili tuweze kusomesha wanafunzi wengi zaidi.
Mkuu hapo unakosea Cuba accomodation ni free na zipo vyuoni, msosi wa serikali, vitendea kazi vyote bure except for few private students coming from other countries. Sasa hapa msosi hamna, accomodation hazitoshi na chache zilizopo zinalipiwa. Ukikaa nje ya chuo kuna ishu ya nauli. Kumbuka uchangiaji upo wa kiaina maana nauli ya kutoka kwenu kanyigo unajilipia, hata hizo hela za mkopo hazireflect market price ya chakula na bei za kurent nyumba hivyo basi the rest unachangia, siku hizi facuulty requirements unajitegemea, na kumbuka maisha si accomodation na chakula tu!
Mkuu hapo unakosea Cuba accomodation ni free na zipo vyuoni, msosi wa serikali, vitendea kazi vyote bure except for few private students coming from other countries. Sasa hapa msosi hamna, accomodation hazitoshi na chache zilizopo zinalipiwa. Ukikaa nje ya chuo kuna ishu ya nauli. Kumbuka uchangiaji upo wa kiaina maana nauli ya kutoka kwenu kanyigo unajilipia, hata hizo hela za mkopo hazireflect market price ya chakula na bei za kurent nyumba hivyo basi the rest unachangia, siku hizi facuulty requirements unajitegemea, na kumbuka maisha si accomodation na chakula tu!
Cuba admission ya university wanapewa kwanza members wa communist party, kama sio mamber unaweza usipate course unayoitaka. Is this what we want to emulate?
Quatitative vs Qualitative change- Ktk Machapisho ya kisayansi na vitabu ktk EA Tz tuko mbali ukilinganisha na Ug au Kenya hata Academics wa Kenya na Ug. wanajua hili. Kenya ubora zaidi ni 'good English'!
Je hii ndio kipimo cha maendeleo ktk elimu ya juu?
What do we need in Tz- Quality or Quantity? Je ni kipi bora?
wewe unatakiwa kubadilika mtazamo wako, au itabidi tuchukue another very effective way za kumlazimisha mtu kama wewe kuelewa na ili siku nyingine uelewe haraka zaidi!
Sijakuelewa kabisa mkuu, nafanya review za mitihani ya Kenyatta university, sikuelewi unaposema kuwa Kenya hakuna quality ya Elimu!! hii notion isiyo sahihi inaletwa na watawala kuwadumaza watanzania.Hivi ili tuonyeshe tuna elimu nzuri kuliko kenya tufanye nini? elimu ni nini hasa? clarify please,kuwa we have good quality ya elimu than kenyans!!!
Ukishindwa kutoa vithibitisho na notion hizo za vijiweni, usiseme tena sentensi hii kwa watu wengine. In short hao wenye elimu ndogo ndio wana mabenki nchini kwenu, wana NGO, organisation mpaka wana miliki magazeti ndani ya nchi yako!, ndio hao managers kwenye foreign companies nyingi ninazozifahamu, ndio wengine tuo Mlimani, I can not mentin their names, we too have professors that they studied in Kenya!
sikuelewi, nini kinatufanya turinge tuna elimu nzuri, kusoma kwa kiswahili darasa la sita na saba!, halafu kurudia kwa kiingereza form one na two??? is that what you are talking???