Hivi bado hujajua kuwa utaratibu mpya wa kutoa mikopo ndio uliokiwezesha chuo cha Tumaini kuongeza idadi ya wanafunzi wake toka 200 mwaka 1997 hadi 8000 mwaka huu? Je hizi sio jitihada zinazostahili pongezi?
Wakati mwingine watanzania sijui tumelogwa ama vipi. Hebu tuangalie takwimu hizi.
Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru idadi ya magraduates tulio kuwa nao ilikuwa 571 na tulikuwa watu karibu milioni tisa.
Mwaka 1963 Kenya ilipopata uhuru miaka miwili baadaye ilikuwa na jumla ya graduates 711 kwa watu karibu milioni saba.
Mwaka 1990 idadi ya waliokuwa wanajiunga na Chuo Kikuu nchini Tanzania ilukuwa karibu 3,000 wakati Kenya ilikuwa 30,000.
Mwaka 2000 (baada ya miaka 40 ya uhuru) jumla ya magraduates wa Tanzania ilikuwa karibu 40,000 kwa watu karibu 32,000,000 - ikiwa na maana ya graduate moja kwa kila watu 1,000 !!
Huo huo mwaka 2000, Kenya walikuwa na graduates zaidi ya 200,000 kwa watu karibu milioni 30,000,000 sawa na graduates moja kwa kila watu 150 !!
Inawezekana hizi takwimu si sahihi 100% lakini zinatoa mwanga jinsi sera zetu za elimu zilivyotudumaza. Halafu bado hatuoni umuhimu wa kutafuta njia bora za kuwasomesha wanetu badala yake tunatumia FFU kuzima manung'uniko yao. Uhazili wa wanafunzi Chuo Kikuu unafanywa chini ya uangalizi wa polisi walioshika bunduki.
Hapa Afrika Mashariki tu, tunaongoza kwa ujinga - je huko kwingine ? Inahitaji moyo kujaribu kutetea hali kama hii hata kwa muumini wa utulivu na amani. Kwa kukosa elimu tumeshindwa hata kuchagua kilicho bora.
Quatitative vs Qualitative change- Ktk Machapisho ya kisayansi na vitabu ktk EA Tz tuko mbali ukilinganisha na Ug au Kenya hata Academics wa Kenya na Ug. wanajua hili. Kenya ubora zaidi ni 'good English'!
Je hii ndio kipimo cha maendeleo ktk elimu ya juu?
What do we need in Tz- Quality or Quantity? Je ni kipi bora?

Tanzania iko nyuma sana ya Kenya kwenye uandishi wa vitabu. Hatuna watu kama Ngugi wa Thiongo!
Quality education unayozungumzia Tanzania iko wapi? Umesahau hali halisi ya madarasa, waalimu, maktaba, maabara, etc ilivyo Tanzania? Kenya ni nafuu
Maswala ya msingi kwenye hii mada ni:
(1) Kuna umuhimu wa serikali kuwapa wanafunzi mikopo kwa asilimia 100?
(2) Uwezo wa serikali kufanya hivyo upo?
Jibu la swali la kwanza linaonekana toka kwenye michango ya wengi. Katika nchi masikini na ambayo kiwango cha elimu bado kiko chini sana, ni vizuri Taifa lisomeshe vijana wote wanaochaguliwa kuingia vyuo vikuu. La sivyo watasoma watoto wa matajiri tu, na hao ni wachache mno!
Jibu la swali la pili linahitaji takwimu. Hotuba ya Bajeti ya Elimu ya 2008 - 2009 (ipo kwenye website a serikali) inatoa takwimu za vijana walioko kwenye Elimu ya Juu kama 65,966. Kurahisisha, tufanye 66,000. Ada wanayodaiwa na vyuo ni shilingi 2.7 million kila mmoja (Hiyo ni ya UDSM, na nimeweka link yake kwenye ukurasa wa 16 wa thread hii).
Ukizidisha idadi ya wanafuzi (elfu 66) kwa kasi cha ada (2.7 mi.) zinafika 178 billion shillings. Hizo ni17.8% ya bajeti yote ya Elimu ya mwaka huu.
Swala basi ni hili: serikali ina uwezo wa kutumia 178/=bn kulipia wanafunzi wa Elimu ya Juu? Ndiyo. Hizo ni kama nusu ya fedha zinazokusanywa na TRA kwa mwezi.
66,000. Ada wanayodaiwa na vyuo ni shilingi 2.7 million kila mmoja (Hiyo ni ya UDSM, na nimeweka link yake kwenye ukurasa wa 16 wa thread hii).
Ukizidisha idadi ya wanafuzi (elfu 66) kwa kasi cha ada (2.7 mi.) zinafika 178 billion shillings. Hizo ni17.8% ya bajeti yote ya Elimu ya mwaka huu.
Swala basi ni hili: serikali ina uwezo wa kutumia 178/=bn kulipia wanafunzi wa Elimu ya Juu? Ndiyo. Hizo ni kama nusu ya fedha zinazokusanywa na TRA kwa mwezi.
Hesabu zako haziko sahihi.
Kiwango kinachohitajika ni sh. bilioni 1200. Bajeti ya wizara ni sh. bilioni 1080.Wewe umehesabu wanafunzi wa vyuo vya serikali tena wa ngazi ya shahada peke yao. Elimu ya juu inajumuisha stashahada pia. Halafu umeconsider wanafunzi walio nchini tu, wale wa Ukraine mliokuwa mnapiga kelele serikali iwasaidie sasa hivi unajifanya umewasahau, na si Ukraine peke yake, karibu kila nchi kuna wanafunzi wanaowezeshwa na serikali. Juzi tu mlimsikia Dr. Slaa akimwomba balozi wa Tanzania nchini Urusi ajiuzulu kwa kutokuwasaidia wanafunzi kupata mikopo yao mapema. Unafikiri asilimia 100 ya mahitaji ya mwanafunzi wa Urusi ni sawa na ya mwanafunzi wa UDSM? Leo hii mnajifanya mnatoa mahesabu hayo katika pesa zinazohitajika? kweli mna lengo zuri na taifa letu nyinyi??? Hebu elezeni vizuri, nyinyi mnaotaka asilimia 100, mnataka hizo asilimia 100 wapewe wanafunzi wote wa kitanzania au wanafunzi wote wa vyuo vya serikali? mnapaswa kuweka hili bayana maana kama hesabu mnazopiga ni za vyuo vya serikali tu mnaanza kuonyesha dalili ya kujali wanaosoma kwenye vyuo hivyo peke yao!
Jamani hakuna haja ya kufanya propaganda katika jambo ambalo linawaathiri watu moja kwa moja. Hawa vijana hawapati elimu bora kwa sababu ya hii migomo isiyo na msingi wowote. Wapeni ushauri waelewe nini wanapaswa kufanya. Msiwasukume kwenye sakata la migomo halafu mkabaki kuwaangalia kama sinema.
Swali la kizushi:
Hivi kuna nchi gani INAYOENDELEA(meaning Least Developed Countries) yenye population ya ZAIDI ya milioni 30, inayowapa wanachuo wake WOTE grant ya 100%?
Tukishaijua, tutaweza kujifunza a thing or two kutoka kwao.
Mkuu Nyambala,
Statistics za cuba on social services are highly impressive, no doubt!... sasa kama population yao 2008 ndio wako milioni 11.8, sijui huko 1970 or 1980 walikua wangapi.
Im am not trying to take anything away from sera nzuri zenye results walizonazo. Na naamini there are man things za kujifunza kutoka kwao, no doubt. Ila numbers do matter... Pamoja na kuitwa least developed lakini Cuba GDP per capita yao ni USD 12,700 wakati ya kwetu ni 1,300(CIA world fact book), that is ten times ile ya kwetu.
I am not sure kama huu ni mfano comparable na sisi. But thanks for the informative and awe inspiring posts on cuba.