MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,710
- 1,660
Nilipewa dhaman ya kuwasajili hawa tukiwa na junior wenzangu kama 4. deadline ilipofika, hapo ndipo mwanzo wa picha nzima nilivyoipata.
Binti akiwa amevaa ushungi, mtoto mdogo amefaulu kutoka shule moja maarufi ya special school, akija ukweli akiwa anatoa machozi! alisema anasubiri wapewe mikopo na serikali, katika ule mkopo (posho ya chakula)atakaopewa ndio atakayokata alipe asilimia 40 anayodaiwa! mimi ni mtu mzima, na ndoa yangu changa, nilimwacha yule binti pale na kwenda chooni kutoa machozi kidogo. nikamuuliza sasa utakula nini? akasema sijui, kwao morogoro, dar hana ndugu, ila kuna watu anatoka nao kijiji kimoja, labda atakuwa akienda kwa katika nyakati za shida.
Nilimsikiliza wa pili,wa tatu, wa nne, mpaka wote 20. Moyo wangu ulijaa simanzi.
Kama leo kuna mtanzania yoyote bado anakubali ile kauli kuwa serikali haina uwezo wa kutosha basi huyo atakuwa anaishi kwenye dunia nyingine, yaani dunia ya ksadikika. Tunaweza kununua magari ya kifahari abayo hata serikali ya Japan yenyewe yanakotoka magari hayo hainunui, tunaweza kumpa kila waziri mashangingi mawili wakati waziri wa nchi kama Uingereza hawezi kutembelea gari kama hilo, sijui tunategemea nini. Tuna mdanganya nani tunapoema serikali haina uwezo wa kutosha, ni uwezo gani huo? Kama Mr Kagoda peke yake anaweza kukwapua mabilioni ya shilingi, nani anaweza kuamini kaul ya kuwa hatuna uwezo? Huu sio mwaka 84 au sio kipindi ch Mzee Ruksa ambapo serikali haikuwa na uwezo. Mkapa aliweka msingi mzuri wa kuifanya nchi iwe na pesa na inazo mpaka wenye uchu wanaiba Kwa hiyo ni lazima serikali i-invest kwenye elimu.
Sasa swali ulilopaswa kujiuliza wewe kama mwalimu ulioona wanafunzi wenye hali ngumu mpaka ukalia ni je, kwa nini wanafunzi wenye hali ngumu wanakubali kugoma kudai kila mwanafunzi apewe asilimia 100 wakati wanajua kuna wenzao wenye uwezo wa kujisomesha. Na kwanini hujiulizi wanafunzi wenyewe kwa wenyewe kwanini wasiripoti hao wanafunzi walioandikwa kuwa wana asilimia 60 na kupewa asilimia 100??? Je kwanini wanafunzi wanaamini in the solidarity ambayo haipo? Kama kuna solidarity basi wale wenye uwezo wasingeenda hata kuomba huo mkopo, Kama kuna solidarity wale waliopewa mkopo mkubwa kuliko mahitaji yao wangeripoti, kama kuna solidarity basi wanaosaliti solidarity wangeshughulikiwa. Ukweli ni kwamba mtu mwenye hali ngumu kama uliyoelezea hapa hawezi kuwa kiongozi wa mgomo hata siku moja. Viongozi wa mgomo huwa ni watu wenye alternatives.
Kuna kijana ninamfahamu alikuwa ana fujo sana shuleni. Alikuwa anaorganise migomo na fujo nyingi tu. Huyu jamaa ni mtoto wa kiongozi wa juu serikalini. Baba yake alikuwa hataki akasome nje ya nchi, sasa jamaa alikuwa anatafuta mbinu za kufukuzwa mlimani ili apate sababu ya kupelekwa kusoma nje!!! Sasa vitu kama hivi ndio hawa wanafunzi wanapaswa kuvitambua. Mtoto wa masikini anapata wapi nguvu ya kukataa kujaza form ya kurudi chuo?? Kwanza ndugu zake watamuelewa?
Kuna jamaa mwingine alikuwa nachukua mkopo bodi na hataki baba yake ajue kama ameomba mkopo, kwa sababu baba yake pia anampa mahitaji yake yote ya chuo. Sasa ni akili gani mnayoitumia kutaka kila mtu apewe asilimia 100?? Wewe kama ni mtetezi wa wanyonge unapaswa kutetea wanyonge wapewe asilimia 100 na ili hilo litokee ni lazima idadi ya wanaopewa mkopo iendane na uwezo uliopo, the best way to cut the number ni kuwatoa wenye uwezo wa kujilipia kwenye mahesabu ya mkopo.
Swala la TV nimetumia kama mfano tu, samahani kama limekuoffend fellow.
Still you are analyising things that are not practical! huo si ubinadamu unachotaka ni kulazimisha! haipo hiyo go anywhere duniani. Si kweli kuwa wale wenye uwezo waseme kuwa hatutaki mkopo! that beyond humn nature as far as i know them, people always want to have more! situation ingekuwa worse kama usingekuwa mkopo. hawawezi kuwa punished kwa sababu wanazo! ningekuwa mimi ningewabana kurudisha na pengine hata kurudisha kwa interest. Mkuu nakatwa sh. 11,000 kila mwezi kulipa deni hili la chuo kwa miaka 10, kipato ninachopata kwa sasa ni kikubwa kiasi ambacho hata wakisema wakate with interest, hata wakondoa 20,000 kila mwezi no problem!!
Hayo matatizo mengi wanafunzi viongozi wameripoti na serikali inajua hivyo, wakiwa serious inabidi waunde tume wapitie nyarak zote kuhakiki! it is costful, the only way wape asilimia 100!
Kama nitakuwa upande wako ku-promote hili swala, maoni yangu ni kuwa we need critical thinkers wewe na mimi tusadiane katika hili swala, ebu angalia
1. Serikali ilitakiwa kujitayarisha katika hili swala, kujiyatarisha huko kuendane kubadilisha mfumo wa elimu ambao utemuwezesha mtanzania anayemaliza kidato cha sita, kujiajiri, kuwa trainable katika post mbalimbali kazini.
2. Kuondoa barrier ya kupata kazi kwa hawa wanafunzi, wenzetu ulaya hususan nchi kama canada niliyopata wahi soma, kuna kitu wanahita summer job, to my surpirise mpaka watoto wadogo utawakuta wakipiga kazi sehemu mbalimbali kuongeza kipato, because they ar education is good
3. Kujitayarisha kwa serikali kuendane na ku-promote vyuo vingi ambavyo vitazalisha wataalamu kwa bei nafuu, katika mikoa mbalimbali, this is possible, if we need to build our country na sio kurely tu kwenye university as if mtu pekee anayetakiwa makazini lazima atko mlimani!
4. Vyuo vyote vya elimu ya juu vinatakiwa viondoe kitu kiachoitwa disco, hii itamfanya mwanafunzi asome kama anatka kusoma, afanye kazi katika nyakati asizo na fedha. suprising canada kwa mfano wanatoa asilimia 100 ya mkopo , lakini wanafunzi wengi wanafanya kazi na wanajisomesha , HII INAPELEKEA BODI YA MKOPO HUKU KUTANGAZA KWENYE MA TV, NA REDIO KUWAVUTIA WATU WACHUKUE MKOPO!!!!!!
Hali ya sasa ya wanafunzi inapelekea kutegemea wazazi wao zaidi wengi maskini wa kutupwa ambayo nikianza kuwaelezea muda hautoshi.
"" siri hapa ni kuwa hata kikwete hataki iwe hivi ila pressure za donors" na hii ilitakiwa kiongozi anayejali na kutetea watu wake. kwa kuwatayarisha kama nilivyoelezea hapo juu.
waberoya
"" siri hapa ni kuwa hata kikwete hataki iwe hivi ila pressure za donors" na hii ilitakiwa kiongozi anayejali na kutetea watu wake. kwa kuwatayarisha kama nilivyoelezea hapo juu. [/COLOR][/B]
waberoya
Sasa swali ulilopaswa kujiuliza wewe kama mwalimu ulioona wanafunzi wenye hali ngumu mpaka ukalia ni je, kwa nini wanafunzi wenye hali ngumu wanakubali kugoma kudai kila mwanafunzi apewe asilimia 100 wakati wanajua kuna wenzao wenye uwezo wa kujisomesha. Na kwanini hujiulizi wanafunzi wenyewe kwa wenyewe kwanini wasiripoti hao wanafunzi walioandikwa kuwa wana asilimia 60 na kupewa asilimia 100??? Je kwanini wanafunzi wanaamini in the solidarity ambayo haipo? Kama kuna solidarity basi wale wenye uwezo wasingeenda hata kuomba huo mkopo, Kama kuna solidarity wale waliopewa mkopo mkubwa kuliko mahitaji yao wangeripoti, kama kuna solidarity basi wanaosaliti solidarity wangeshughulikiwa. Ukweli ni kwamba mtu mwenye hali ngumu kama uliyoelezea hapa hawezi kuwa kiongozi wa mgomo hata siku moja. Viongozi wa mgomo huwa ni watu wenye alternatives.
Kuna kijana ninamfahamu alikuwa ana fujo sana shuleni. Alikuwa anaorganise migomo na fujo nyingi tu. Huyu jamaa ni mtoto wa kiongozi wa juu serikalini. Baba yake alikuwa hataki akasome nje ya nchi, sasa jamaa alikuwa anatafuta mbinu za kufukuzwa mlimani ili apate sababu ya kupelekwa kusoma nje!!! Sasa vitu kama hivi ndio hawa wanafunzi wanapaswa kuvitambua. Mtoto wa masikini anapata wapi nguvu ya kukataa kujaza form ya kurudi chuo?? Kwanza ndugu zake watamuelewa?
Kuna jamaa mwingine alikuwa nachukua mkopo bodi na hataki baba yake ajue kama ameomba mkopo, kwa sababu baba yake pia anampa mahitaji yake yote ya chuo. Sasa ni akili gani mnayoitumia kutaka kila mtu apewe asilimia 100?? Wewe kama ni mtetezi wa wanyonge unapaswa kutetea wanyonge wapewe asilimia 100 na ili hilo litokee ni lazima idadi ya wanaopewa mkopo iendane na uwezo uliopo, the best way to cut the number ni kuwatoa wenye uwezo wa kujilipia kwenye mahesabu ya mkopo.
Swala la TV nimetumia kama mfano tu, samahani kama limekuoffend fellow.
Kijana sijui unaingelea zama zipi ulizomaliza from six.....i think ni 90's au mwanzoni mwa 2000...mkuu hii ni Tanzania njoo ujionee na sio kusoma kwenye blogs na Jf peke yake....Kama degree holder mwenye proffesional anakosa ajira hata ya 70k kwa mwezi iweje kijana wa form 6 HGL apate ajira....1. Mwanafunzi aliyemaliza form six anaweza kujiajiri. Nakumbuka mimi nilivyomaliza form six sikuwa kijiweni! nawafahamu wengi tu wanaofundisha tuition au kufanya business baada ya kumaliza form six. Siyo kwel kwamba mwanafunzi aliyemaliza form six hawezi kujiingizia kipato.
Mkuu unanisikitisha kweli kweli......niambie makampuni gani tanzania yanayotoa kazi za summer?? na kama yapo nakuapia hawawezi kuajili watu wasiokuwa na ujuzi.....2. Hizo kazi za summer hutolewa na makampuni binafsi. Makampuni kama hayo Tanzania yapo na yanapenda kutoa kazi kwa wanafunzi, je wanafunzi wangapi hutafuta kazi wakati wa likizo? Huko Cadana na nchi nyingine zilizoendelea siyo serikali inayoandaa kazi za summer kwa wanafunzi. Huwa kuna recruitment agents ambao wanaunganisha wanaotafuta kazi na wanaotafuta wafanyakazi. Hivyo basi kutokuwepo kwa kampuni za aina hii Tanzania isilaumiwe serikali tu. Huu ni mwanya wa ujasiriamali kwa kila mtanzania, tusipofanya hivyo watakuja wa afrika kusini kufanya biashara hiyo.
Tusiegemee kwenye kulaumu tu!
Mkuu hebu tafuta data kwanza....vyuo vingapi vya binafsi na wanafunzi wangapi wamepata mikopo...hizo ni piga domo za serikali ya tanzania tumezoea mara ngapi wanasema mkakati mkakati mkakati toka enzi ya nyerere mpaka leo vikao vya mikakati..lini itatekelezwa??ad 3. Ukipata fursa, tafadhali ipitie hotuba ya waziri wa Elimu kwenye bunge la bajeti. Huu ni mkakati ambao serikali inautekeleza kwa miaka kadhaa sasa. Mojawapo ya utekelezaji wake ni kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo binafsi pamoja na kuanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa vyuo hivyo.
Nimegundua wengi humu mmesoam majuu au mnaishi majuu mnakuja bongo krisimasi na mwaka mpaya mnatimua......mkuu hali ya bongo unaisoma Ippmedia na JF tu.....hiyo subira unayosema ilianza lini kusubiriwa??Hata hivyo ni muhimu kuwepo na subira, kwa sababu kumridhisha kila mtu kwa mpigo wakati mwingine huwa ni ngumu. Sasa hizi tabia za wanafunzi kusioridhika kuamua kuwa hakuna kitachoendelea chuoni mpaka yale wanayotaka wao yatekelezwe yanadhihirisha kutokukomaa kiakili.
ngrrrrrrrrrrrrrr nachoka kabaisa.......this is too lowHivi tunategemea kupata great people among watu ambao wanaona ni bora kununua TV kuuuubwa kuliko kujilipia ada? Hivi kuna haja gani kila mwanafunzi awe na TV yake pale mlimani. Je, TV Moja haitoshi kwa block nzima ya wanafunzi ambao wanaclaim kuwa ni masikini???
Kijana sijui unaingelea zama zipi ulizomaliza from six.....i think ni 90's au mwanzoni mwa 2000...mkuu hii ni Tanzania njoo ujionee na sio kusoma kwenye blogs na Jf peke yake....Kama degree holder mwenye proffesional anakosa ajira hata ya 70k kwa mwezi iweje kijana wa form 6 HGL apate ajira....
Niambie mfano wewe umaliza from 6 leo hii 2008...umekosa nafasi ya kuingia chuo chopchote tanzania.....unatafuta kipato(kujiajiri) utaanzaje????? Nisaidie mkuu
Mkuu unanisikitisha kweli kweli......niambie makampuni gani tanzania yanayotoa kazi za summer?? na kama yapo nakuapia hawawezi kuajili watu wasiokuwa na ujuzi.....
mkuu unalinganisha Canada na Tanzania????
Anyway wewe kama Mtanzania hebu ishauri basi serikali na wajasiriamali wengine maana unasema serikali isilaumiwe......
Mkuu hebu tafuta data kwanza....vyuo vingapi vya binafsi na wanafunzi wangapi wamepata mikopo...hizo ni piga domo za serikali ya tanzania tumezoea mara ngapi wanasema mkakati mkakati mkakati toka enzi ya nyerere mpaka leo vikao vya mikakati..lini itatekelezwa??
Nimegundua wengi humu mmesoam majuu au mnaishi majuu mnakuja bongo krisimasi na mwaka mpaya mnatimua......mkuu hali ya bongo unaisoma Ippmedia na JF tu.....hiyo subira unayosema ilianza lini kusubiriwa??
Kusbiri gani huko kama hao wanaosema tuwasubiri wananunua gari la mil 100 4WD kwa matumizi ya Dar....
wawasubiri vipoi wakati hao hao wanajilimbikizia bilions of money nje na wanaviita vijisenti....
wawasubiri vioi hao hao....shit!
mkuu jiulize kwanini katika EA Tanzania inatoa wahitimu wachache?
Yes tanzania haitakalika
Hizo tuition kumbe ndio unazosemea?Wanafunzi ninaokwambia wanajiajiri kwa tuition etc. ninawajua live na sizungumzii hadithi. Hivi kuna watu wangapi wenye elimu chini ya form six dar es salaam lakini wanashughuli zinazowaingizia kipato? Elimu waliopata wao ina tofauti gani na ya wanafunzi wa UDSM mpaka imfanye mwanafunzi wa UDSM ashindwe na yule wa mtaani aweze kujitafutia kipato?
mkuu unafahamu wanafunzi wangapi waanaacha masomo kwa kukosa hiyo %? nina ushahidi kwa hiliTanzania imekuwa ikitoa graduates wachache kwa sababu vyuo vikuu vilikuwa vichache, sasa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi idadi ya vyuo inaongezeka na kama unafuatilia statistics utagundua kuwa we are improving kwa mwendo mzuri. Iwapo tutaacha kuwawezesha wanafunzi wa vyuo binafsi kama wanavyotaka wanafunzi wabinafsi wa UDSM basi hatutaweza kufikisha idadi inayolingana na nchi tulizo nazo jirani.
Hivi wanafunziw a udsm hawataki wanafunzi wa vyuo binafsi????? sikujuaIwapo tutaacha kuwawezesha wanafunzi wa vyuo binafsi kama wanavyotaka wanafunzi wabinafsi wa UDSM basi hatutaweza kufikisha idadi inayolingana na nchi tulizo nazo jirani.
Hizo tuition kumbe ndio unazosemea?
kwa muda upi ataweza kupata darasa la kufundisha tuition?
Na pesa ngapi utapata?
Na ni location gani unayoisema? dar nafikiri.....
alafu mkuu tuzungumzie wanafunzi wote sio udsm peke yao.......
Suala la nyie wa nje msikilizwe ni jema sana na si kosa la watanzania ni kosa la viongozi wenu mliowapa dhamana ya kutawala....nenda leo useme una degree ya ulaya na unaweza kazi uone kama hutarogwa au kuundiwa skendo na kupotezwa mazima kazini...
Yaani unataka kusema wanafunzi wa Tanzania wana ratiba ngumu kuliko wanafunzi wote duniani wanaopata muda wa kufanya vijikazi??? Sidhani kama muda unakosekana iwapo kuna marengo.
Pesa wanayopata wanaofundisha tuition ni kubwa kuliko watu walioajiriwa na wizara. Ukiwa na wanafunzi kumi, kila topic unapata zaidi ya sh. laki moja. Hii ni asimilimia 10 ya ada kwa UDSM. Ndugu yangu amesoma hapo na amekuwa anafundisha at the same time, sasa amemaliza chuo na anaendelea na masters kwa mtindo huo huo so kusema kuwa haiwezekani sio ukweli. Yeye hajaajiriwa na ameoa mke! I have seen that it is possible from my own family.
Hivi sasa tunajadili mgomo wa UDSM ndio maana natoa mifano ya UDSM.

Unatania au upo serious!!!!!!!!!? Hahahahahahaaaa
Mkuu kwenye swala la tuition umechemka kabisa tena haufahamu tuition ni kiasi gani. Nikiwa TZ, tena mwakajana nimefundisha (Advance maths & Basic maths) tuition hapo DAR, jamaa zangu wapo mwenge, makumbusho, kumbukumbu mwembeni n.k huwa tunawasiliana. Hiyo laki moja unaipata kama unafundisha door to door kwa watoto wa waheshimiwa/wakubwa/mafisadi. Tembea DAR yote, hiyo hela haipo.
Unakazania tuition, wewe umeshawai fanya tuition? Unajuwa ni masomo gani zaid yanapewa kipaumbele na School candidates na Private candidate?
Samahani mkuu, kwa swala la tuition, umechemka. nakupa 1 out of 100. Huifahamu tuition ya laki moja per topic. Eti nifundishe Set (Form two -maths) kwa laki moja; Tanzania au ????
Unajua bei ya huduma uamuliwa na mtoa huduma, ndio maana soda mlimani city ni sh. elfu moja wakati mtaani ni sh. 400.
Ninajua wanaofundisha topic kwa sh. elfu 20 ndio maana nimesema wanafunzi watano unapata laki kwa topic. Hata kwa wanaoamua kujifanya cheaper wanaweza kupata hiyo elfu 30, haiko mbaya.
Halafu kumbuka kuwa tuition ni mfano tu, kazi za kufanya ni nyingi. kuna aliyetoa mfano wa kusafisha bustani za chuo etc. Hili kuna siku niliwashauri wanafunzi wa muhimbili, wakaniambia hawawezi kusafisha muhimbili watajiaibisha! Well, hii ndio attitude ya wanafunzi wa chuo kikuu Tanzania unfortunately.
Kuna wanaoweza kupika, wangeweza kuanzisha huduma ya ''dada ntilie'' etc.
Yaani shughuli ziko nyingi. Iwapo kuna watu darasa la saba town wanaishi fresh, huwezi kuilaumu elimu eti imeshindwa kukuwezesha kujitegemea.