Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
TANZANIA HAINA BUNGE, ........!!
Nilishasema mara kadhaa suala hili kwa hoja tofauti tofauti, leo narudia tena..... Kama unaamini kuwa Tanzania ina kitu kinaitwa BUNGE kama mhimili , basi unatakiwa ukapimwe akili.
Kwa mfumo tunaoutumia sisi, ili kuwe na BUNGE imara, ni lazima kuwe na Kambi ya Upinzani Bungeni ambayo ni imara. Ili kambi hiyo iwe imara, inapaswa kuwa huru kutoa na kueleza maoni yake juu ya mipango ya serikali, ili kambi hiyo iwe huru, haipaswi kuingiliwa na mtu yoyote katika kueleza kile inachokiona kuwa ni sahihi na muhimu kwa taifa.
Sasa haka katabia kanakoendelea huko Bungeni , ka ofisi ya BUNGE kwa kushirikiana na serikali ya CCM, pamoja na kambi ya CCM ili kumfurahisha MKATA UMEME wa Magogoni aliyezuia BUNGE LIVE, ku-edit hotuba za Kambi ya Upinzani Bungeni kanamaanisha nini?????
Yaani Kambi ya Upinzani Bungeni inakaa, inaumiza kichwa, inafanya tafiti, inakuja na maoni yake ambayo siyo MATUSI, halafu anatokea kichaa mmoja anajiita sijui AG, anaamrisha kiti kilazimshe hotuba ya Upinzani ipanguliwe...... Na inakuwa hivyo, hapo uhuru wa Kambi ya Upinzani uko wapi????
Yaani wao tu ndo wanaotaka wawe wanasikika na data zao za kupika (ooo ndani ya mwaka JEIPIEM viwanda 20,000 vimejengwa), lakini Upinzani ukitaka kuwaeleza ukweli wanafosi ku-edit hotuba zao.
Bahati mbaya BUNGE lenyewe hatuoni, yaani mwaka huu hata ule mpango kuoneshwa marudio usiku wa manane, haupo. Kwahiyo wawakilishi wetu eti wanajadili na kupitisha bajeti kwa ajili yetu, halafu hata sisi wenyewe hatujui kilichomo kwenye hiyo, bajeti.
Halafu BUNGE lenyewe lipo kiganjani kwa MKATA UMEME, yaani akisikia wabunge wake wanaungana na Upinzani kwenye hoja fulani, mfano hoja ya DAUDI, anawaita fasta kuwaonya na kuwatishia kuwakata kwenye uchaguzi ujao.
HATUNA BUNGE TANZANIA, TUNA KUNDI LA WATU WANAOITANA WAHESHIMIWA, MAALUM KWA AJILI YA KUTAFUNA POSHO. HAKUNA LA MAANA