Hivi hakukuwa na nyumba nyengine nzuri za thamani ndogo kidogo?
Manake hiyo payback period sijui ni miaka mingapi
why Gaijin? kwanini ya thamani ndogo? ni nyumba ya diplomat remember?
Udiplomat ndio iwe sababu ya kufuja pesa? Lakini sishangai diplomats wetu kutaka makuu, mawaziri wanaishi na familia zao hoteli, why wao wajivunge!
U got it. Kuna kitu kinaitwa "kustahili"; ukiwa katika nafasi fulani ya utumishi wa umma una "stahili" vitu fulani fulani hivi. Sasa tofauti kubwa iko tu katika kiwango cha mastahili. Katika Tanzania watu pekee wasiostahili vitu fulani fulani ni wakulima tu. Labda kwa sababu hawana nafasi ya kudai mastahili yao na hakuna kupanda vyeo kwenye kulima.
Mlitaka tuendelee kupanga? Ama kweli Watanzania hatuna jema.
Kununua nyumba maana yake hizo fedha bado ni zako, kwani ukiamua kuiuza pengine zinarudi zote na zaidi, inategemea na soko. Jee Kupangisha?
Sasa watueleze nyumba kama hiyo hapo ilipo ikiwa kupangishwa ina pangishwa kiasi gani? sio kuleta habari za upand mmoja tu.
Tanzania ilishamua siku nyingi kuwa kila itapopata wasaa itakuwa ikinunua nyumba zake za ubalozi nje, cha kushangaza ni nini?
Ni jambo jema sana la kujivunia. hapo tunauhakika hata kama kodi hatuna hakuna wa kutunyanyasa, ni kitu chetu wenyewe. Hongera sana Serikali.